Timu ya taifa ya soka ya
Tanzania kwa vijana wenye umri wa miaka 20 imesonga mbele kwenye safari
ya kufuzu kwa Fainali za Kombe la mataifa baada ya kuilaza Kenya kwa
mikwaju ya Penalti 4-3 kwenye mechi ya marudiano iliyochezwa kwenye
uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Mechi hiyo imelazimika kuingia hatua ya Penalti
baada ya kumalizika dakika 90 mechi ikiwa sare ya 0-0 na ndipo Tanzania
ilipopata ushindi unaoisogeza kwenye raundi ya pili ya michuano hiyo
inayofanyika kila baada ya miaka miwili.Nalo Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF limemtangaza rasmi kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya soka ya Tanzania Taifa Stars Martinus Ignatius Nooij ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuionoa timu hiyo huku kibarua chake cha kwanza kikiwa tayari kimeishatangazwa ambapo Taifa Stars itashuka dimbani dhidi ya Zimbabwe mwezi Mei mwaka huu kwa mechi ya awali ya kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa zitakazofanyika mwakani nchini Morocco mwezi Februari mwakani.
Tayari Kocha ametangaza majina ya wachezaji tisa wapya kuimarisha kikosi hicho huku beki maarufu wa timu ya Yanga, Kelvin Yondan akitemwa kwenye kikosi hicho baada ya kugoma kuripoti kambini, pasipo kutoa sababu za msingi za kutofanya hivyo.
Katika safari ya kuelekea Morocco hapo mwakani, Uganda itashuka dhimbani dhidi ya Madagascar,huku Burundi ikicheza dhidi ya Botswana,na Harambee Stars ya Kenya itapepetana na Commoro,nayo Rwanda ikicheza dhidi ya Libya.
0 comments:
Post a Comment