Chelsea wamewapa pigo kubwa Liverpool na ndoto yao ya kutwaa Ubingwa wao wa kwanza katika Miaka 24 na wao kujiwekea matumaini baada ya kushinda Bao 2-0 Uwanjani Anfield wakiwa wamechezesha ‘Kikosi hafifu’ huku jicho lao likiwa kwenye Mechi yao ya Marudiano ya Nusu Fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya Jumatano Uwanjani Stamford Bridge.
Mashabiki wa Liverpool walikusanyika kwa
ajili ya Mechi hii wakiwa na hakika ya ushindi, hasa baada Jose
Mourinho kudokeza atachezesha ‘Kikosi hafifu’, na kabla ya Mechi kuanza
Basi lililobeba Wachezaji wa Liverpool lilipokuwa kwa shangwe kubwa nje
ya Anfield mithili ya Paredi ya Ubingwa.
Pengine huu ndio Msemo wa kule kwetu Mwaneromango: “WACHEKELEA MBELEKO, MWANA BADO!”
Bao zilizoiua Liverpool zilifungwa na
Demba Ba katika Dakika ya 45 baada ya Nahodha Steven Gerrard kuteleza na
Demba Ba kunufaika na kwenda kufunga na la Pili kupigwa Dakika za
Majeruhi na Willian, alietokea Benchi, alipopokea Pasi murua ya Fernando
Torres.
Ushindi huu umewaacha Chelsea wakiwa
Pointi 2 nyuma ya Vinara Liverpool lakini huenda matokeo haya
yakawanufaisha sana Manchester City ambao wana Mechi mbili mkononi na
wakishinda zote wataikamata Liverpool na kuongoza kwa Ubora wao wa
Magoli.
MATUKIO MBALIMBALI KWENYE MECHI HIYO
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari za michezo pamoja na picha za mchezo huo kwa wakati muafaka bila zengwe
0 comments:
Post a Comment