Facebook

Sunday, 27 April 2014

Basi la RATCO lapata ajali mbaya huko kibaha,Pwani...........

 

Ilikuwa ni purukushani wakati ambapo kila abiria akijaribu kujikwamua na kutoka nje ya basi hilo



 
 
Basi la kampuni la RATCO linalofanya safari zake Dar-Tanga limepata ajali baada ya ktumbukia mtaroni maeneo ya Kongowe,Kibaha mkoani Pwani jion ya leo
Kwa mujibu wa shuhuda ambaye ni mdau wa katemimethsela.blogspot.com aliyeongea na sisi kwa njia ya simu anadai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni baada ya gari ndogo kuchomoka tairi lake na kisha kwenda kukanyagwa na basi La RATCO na kisha basi hilo kwenda kuanguka na kulalia ubavu wa kushoto.

Namshukuru mdau huyu kwa kutupatia habari nyeti kama hizi kwa wakati na muda muafaka.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari za kina kwa wakati na muda muafaka kutoka kwa wadau wetu waliosambaa karibia mikoa yote nchini Tanzania..

0 comments:

Post a Comment