Monday, 28 April 2014
Ajali mbaya yatokea Iringa,Abiria 38 wajeruhiwa.......
Taxi ambayo nayo ilisababishiwa ajari ikiwa katika eneo la tukio, huku askari polisi wakilinda usalama wa mali za abiria na baadhi ya vitu katika eneo la tukio.(P.T).
Daladala aina ya Coster yenye namba za usajiri T.960 AQY inayofanya safari zake za Kibwabwa mjini Iringa mara baada ya kugongana na gari aina ya Isuzu Tipa, lenye namba SM 3363 katika Mlima wa Ipogolo eneo la Kisima cha Bibi.
BASI aina ya Coster linalofanya ruti zake Kibwabwa Manispaa ya Iringa likiwa eneo la tukio, baada ya kugongana na Roli Tipper na kusababisha ajali iliyojeruhi zaidi ya watu 30. ZAIDI ya abiria 38 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari manne mjini Iringa, baada ya Bus dogo la abiria aina ya Coster kufeli breki na kuyagonga magari matatu, ajali ambayo imetokea majira ya saa saba mchana wa siku ya jana. Tukio hilo limetokea katika mlima wa Ipogolo, eneo maarufu mjini Iringa kama "Kisima cha bibi", ambapo ajali hiyo imesababisha majeruhi 38 ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Iringa, huku chanzo cha ajali hiyo kikisemekana kuwa na kuferi breki kwa Bus hilo la abiria,lenye namba T. 960 AQY na kuyavaa magari matatu, gari kubwa aina ya Tipper Isuzu SM784 BNA la manispaa ya Iringa, Tax pamoja na Hiace. Akizungumzia hali ya majeruhi wa tukio hilo , Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa Dr. Deogratius Manyama amesema wamepokea majeruhi 38, na waliolazwa ni 8 huku majeruhi watatu wakiwa na hali mbaya, na kuwa majeruhi wengi wameumia zaidi kichwani na kifuani, huku majeruhi 27 wakiruhusiwa kurudi nyumba kwao kutokana na kutokuwa na majeraha makubwa.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari mbalimbali zilizojiri maeneo tofauti tofauti kwa wakti muafaka........
Related Posts:
Kilichomuua ‘Mtoto wa Boksi’ Chabainika; wahusika kunyongwa! Kufuatia kifo cha mtoto Nasra, almaarufu kama ‘mtoto wa boksi’, kuna kila dalili kwamba kifo chake kimetokana na maradhi aliyoyapata wakati akiwa anaishi kwenye boksi. Kwa kuwa imethibitika kwamba mtoto alifarik… Read More
BREAKING NEWS:Ajali mbaya ya gari yatokea Chuo Kikuu cha ardhi,wasichana wamkimbia dereva baada ya ajali. Ajali mbaya ya gari imetokea muda si mrefu maeneo ya Chuo Kikuu cha Ardhi katika barabara inayoelekea Makongo karibu na hostel za wasichana (Low Cot). Baada ya gari ndogo aina ya Toyota Vits iliyokuwa imeb… Read More
Sakata la Uda lachukua Sura Mpya,michezo mchafu yafanyika.. Sakata la nani mmiliki halali wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda), limeendelea kuchukua sura mpya. Wakati Mbunge wa Temeke (CCM), Abbas Mtemvu akitoa tuhuma kwamba limeuzwa kinyemela, Mwenyekiti na Mkurug… Read More
Mtoto mchanga auwawa kwa kufungwa Plasta mdomoni na puani kisha kutupwa. Mtoto mchanga, amekutwa ametupwa pembezoni mwa barabara ya Kawe-Beach, huku puani na mdomoni akiwa amefungwa plasta, iliyosababisha kukosa pumzi na kufariki. Katika hali isiyo ya kawaida mwanamke mmoja amba… Read More
Kilichosemwa bungeni juu ya picha chafu zinazosambazwa mitandaoni za watu maarufu. Sakata la kusambaa picha zisizokuwa na maadili mitandaoni zikiwemo za watu maarufu hapa nchini leo limezungumziwa tena katika bunge la Tanzania kule Dodoma ambapo katika kipindi cha maswali na majibu Mhe. Habib Mnya… Read More
0 comments:
Post a Comment