Rais
Jacob Zuma wa Afrika Kusini amekuwa akiongoza sherehe za kutimiza miaka
20 ya demokrasi na kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi.
Akihutubia
taifa Rais Zuma alisema Afrika Kusini inaanza kupona vidonda vya
historia ya ukatili na mgawanyiko na taratibu inajenga umoja wa
taifa.Lakini alisema bado kuna kazi ya kukamilisha lengo la kuondosha
umaskini, tofauti za pato na ukosefu wa ajira.Lakini alisema bado kuna
kazi ya kukamilisha lengo la kuondosha umaskini, tofauti za pato na
ukosefu wa ajira. Sherehe hizo zinafanywa kabla ya uchaguzi mkuu ambapo
chama tawala cha ANC kinakabili upinzani dhidi ya uongozi wa nchi tangu
kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi mwaka wa 1994.
0 comments:
Post a Comment