PASUA
jipu! Mastaa wawili wenye majina makubwa Bongo, mwanamitindo Jokate
Mwegelo ‘Kidoti’ na Mbongo-Fleva Juma Kasim ‘Juma Nature’ wanadaiwa
kuacha mshangao kwa wasanii wenzao baada ya kutifuana, Ijumaa Wikienda
limeng’atwa sikio.Pamoja na kwamba Nature amekuwa akizuga kutomaindi
lakini habari za kushangaza zilidai kwamba mkali huyo wa Temeke amekuwa
akimtuhumu mwanadada huyo kuwa amemuibia wazo lake la biashara ya ndala
au kandambili. Kabla ya madai haya mapya, Nature aliwahi kunukuliwa
redioni wakati akitambulisha wimbo wake mpya wa Chuma Ulete kuwa yupo
mbioni kuingiza bidhaa hiyo sokoni. Madai ya sasa yanaeleza kwamba
Nature amekuwa akilalamika kuwa Jokate ‘amekopi’ na ‘kupesti’ wazo lake
la biashara.Pia ilisemekana kwamba Nature amekuwa akimtafuta Jokate ili
kuweka suala hilo sawa bila mafanikio. “Nature amekuwa akimpigia simu
Jokate lakini haipokelewi,” kilidai chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa
popote hata kwa mtutu wa bastola. Kwa mujibu wa Nature bado
hajabahatika kuziona kandambili za Jokate lakini amekuwa akiambiwa na
watu wake kuwa mrembo huyo kamuibia. NATURE AFUNGUKA Alifunguka: “Hadi
sasa hivi sijabahatika kuziona hizo ndala ila nishaambiwa na watu wangu
wengi tu kuwa Jokate ameniibia wazo langu.“Mimi nasema ni wizi wa ajabu
ambao sikutegemea kama Jokate angenifanyia kitu mbaya. “Kweli
sikutegemea kama ishu kama hiyo ingefanywa na mtu kama yeye (Jokate) ila
hata kama ametoa mimi wazo langu liko palepale.“Nitakuja kuzitoa tu
hizo kandambili zenye picha na jina langu.” |
0 comments:
Post a Comment