CHIPUKIZI wa Manchester United, Adnan Januzaj, atakuwemo kwenye Kikosi cha awali cha Kombe la Dunia cha Belgium kama ilivyohakikishwa na Kocha wa Nchi hiyo Marc Wilmots.
Wiki iliyopita, Marc Wilmots ndie
alietoboa kuwa Januzaj amekubali kuichezea Belgium licha ya kutakiwa na
kuwa na uwezo wa kuziwakilisha Albania, Kosovo, Turkey na Serbia kwa
misingi ya mizizi ya Asili ya Wazazi wake.
Januzaj atakuwemo kwenye Timu ya Belgium
ambayo itapiga Kambi ya Mazoezi Mwezi ujao kujitayarisha na Fainali za
Kombe la Dunia zitakazochezwa huko Brazil kuanzia Juni 12 lakini Kocha
Marc Wilmots amesema hivi sasa hawezi kuahidi kama Kinda huyo atakuwemo
kwenye Kikosi cha mwisho cha Wachezaji 23 watakaoenda Brazil.
Kocha huyo amesema: “Nimemuona mara
kadhaa akicheza na sasa nataka kumuona akiwemo kwenye Kikosi changu.
Atakuwemo kwenye Kikosi cha Awali cha Wachezaji 30 na atakuwepo kwenye
Kikosi cha Wachezaji 26 au 27 ambao watafanya Mazoezi huko Genk na
baadae Sweden. Napenda kuwa na idadi ndogo ya Wachezaji lakini Januzaj
atakuwemo.”
Januzaj, mwenye Miaka 19, alijiunga na
Manchester United Mwaka 2011 akitokea Anderlecht na Msimu huu
amepandishwa na kuwemo Kikosi cha Kwanza cha Timu hiyo na Mechi yake ya
kwanza ilikuwa ya Ngao ya Jamii ambayo Man United waliibwaga Wigan 2-0
Mwezi Agosti Uwanjani Wembley.
Tangu wakati huo amecheza Mechi 32 na kuifungia Man United Bao 4.
Kocha Wilmots alifafanua kuwa
alipokutana na Januzaj na Mawakala wake aliwaambia wazi kuwa uamuzi wa
Mchezaji huyo kuwemo kwenye Kikosi kitakacho kwenda Brazil kitategemea
nini atafanya Uwanjani lakini alidokeza kuwa kuumia kwa Christian
Benteke kumezidisha nafasi yake kucheza Kombe la Dunia.
Wilmots amesema: “Kwa hakika huyu ni
Mchezaji wa kuvutia na hasa baada kukosekana Benteke. Watu wengi hawajui
kuwa akiwa na Timu ya Rizevu ya Manchester United mara nyingi amecheza
kama Namba 9. Kumudu kwake nafasi nyingi ni mali!”
0 comments:
Post a Comment