FC Bayern Munich v Real Madrid CF
-Allianz Arena, Munich, Germany
Rekodi ya Bayern Munich wakiwa Nyumbani kwao dhidi ya Real Madrid ni Ushindi: 8, Sare: 1 Kufungwa: 0.
-Real Madrid wameshinda mara 2 tu katika
safari zao 27 Nchini Germany, mojawapo ikiwa ni ushindi wa magoli 6-1
dhidi ya FC Schalke katika Raundi ya Mtoano ya Timu 16 Msimu huu.
-Bayern wamefanikiwa kupindua vipigo vya
Mechi za Kwanza za Ulaya za Ugenini mara 9 kwa kushinda kwao, lakini
wamefungwa mara 10 zikiwemo mara 7 katika Mechi zao 9 walizocheza mwisho
na kuanza kufungwa Ugenini
-Katika Mechi 6 ambazo walifungwa goli
1-0 Ugenini, Bayern wameweza kushinda Mechi 5 na ya mwisho ilikuwa Msimu
wa 2011/12 walipofungwa na FC Basel kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16
na kuweza kuwatwanga 7-0 katika Marudiano Mjini Munich.
-Real Madrid wameweza kufuzu mara 43 kati ya 56 ambazo walitangulia kushinda Nyumbani kwao.
-Waliposhinda 1-0 Uwanjani Santiago
Bernabéu, Real wameweza kushinda mara 4 kati ya 6 na mara hizo mbili
walizotolewa kwenye Marudiano ilikuwa dhidi ya Juventus, Misimu ya
2004/05 na 1995/96, na mara zote walichapwa 2-0 kwenye Marudiano.
Chelsea FC v Club Atlético de Madrid
-Stamford Bridge, London, England
-Katika Mashindano ya UEFA, Chelsea wamefungwa mara 2 tu kati ya 7 ambazo walitoka Sare Ugenini.
-Wakitoka Sare 0-0 Ugenini, Chelsea
wameshinda mara 1 tu na kufungwa mara 2 na hivi karibuni ni pale
walipotolewa na Barcelona kwenye Nusu Fainali ya 2008/09 walipotoka 0-0
huko Nou Camp na kufungana 1-1 Stamford Bridge.
-Chelsea wameshinda mara 1 tu kati ya 4
walizokutana Nusu Fainali na Klabu toka Spain na hiyo moja ilikuwa dhidi
ya Barcelona Msimu wa 2011/12. Mwaka 2009 walitolewa na Barcelona,
1998/99 walitolewa na RCD Mallorca kwenye Kombe la Washindi la UEFA na
1994/95, walibwagwa na Real Zaragoza.
-Atletico, ambao wamefuzu mara zote
mbili baada kutoka Sare 0-0 Nyumbani, wameshinda mara 1 tu Ugenini dhidi
ya Klabu za England kati ya Mechi 9. Mara hiyo 1 ni pale walipoifunga
Leicester City FC Msimu wa 1997/98 kwenye Raundi ya Kwanza ya UEFA Cup.
DONDOO MUHIMU:
-FAINALI: Estádio da Luz, Lisbon, Portugal 24 Mei 2014
Bayern Munich/Real Madrid v Chelsea/Atletico Madrid
0 comments:
Post a Comment