Wednesday, 30 April 2014
Costa:Najua Chelsea hawatapaki basi,watakuwa wanashambulia,lakini tutawafunga.....
MSHAMBULIAJI hatari wa Atletico Madrid, Diego Costa anaamini kuwa Chelsea hawatatumia mbinu yao ya kujilinda katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya UEFA leo katika uwanja wa Stamford Bridge.
Jose Mourinho alitumia mbinu ya `Kupaki basi` katika mechi ya kwanza uwanja wa Vicente Calderon na kulazimisha suluhu ya bila kufungana na alitumia mbinu kama hiyo kuwafunga Liverpool mabao 2-0 jumapili iliyopita katika mchezo wa ligi.
Hata hivyo, Costa mwenye uraia wa Hispania anatarajia kuona Chelsea ikishambulia zaidi katika mechi ya kesho jumatano kwa malengo ya kufika fainali.
“Sina shaka, ni mchezo mkubwa, acha tufurahi na kuucheza”. Costa amewaambia waandishi wa habari.
“Itakuwa mechi tofauti kwa wenyeji, watajitahidi kucheza kwa kushambulia zaidi”.
Atletico msimu huu wana uchu wa kutwaa ubingwa wa La Liga tangu walipofanya hivyo kwa mara ya mwisho mwaka 1996 na Costa ana ndoto ya kubeba kombe Calderon.
“Ninataka kushinda kombe la ligi na itakuwa furaha kubwa kufanya hivyo mbele ya mashabiki wetu tutakapokutana na Malaga”. Aliongeza.
Atletico Madrid katika mechi bili za mwisho watasafiri kuwafuata Levante na mchezo wa kufungia msimu watakutana na Malaga nyumbani
0 comments:
Post a Comment