Facebook

Wednesday 30 April 2014

Adam Nditi:Niko tayari kuichezea Taifa Stars kama mtakubali uraia wa Nchi mbili...

051c57b47232e95173755dcfe596c530 copy
MCHEZAJI kinda wa klabu ya Chelsea na raia wa Tanzania, Adam Nditi ameilaumu serikali ya Tanzania kuwanyima haki watanzania wengi walio nje ya nchi kuja kuitumikia nchi katika fani mbalimbali kutokana na kushindwa kuruhusu uraia wa nchi mbili.
Katika mahojiano maalum, Nditi amesikitishwa na serikali kushindwa kutoa uraia wa nchi mbili kwasababu wanaona uchungu kuona nchi yao inafanya vibaya wakati wanao uwezo wa kutoa mchango wao.

“Binafsi kama serikali ya nchi yetu itaruhusu uraia wa nchini mbili, niko tayari kuja kuichezea taifa stars hata kesho”. Amesema Nditi.

Nditi ameendelea kufafanua kuwa wapo watanzania wengi wenye fani mbalimbali kama vile wanasoka, madakatari na nyinginezo, lakini wanashindwa kuja kuitumikia nchi kwasababu taifa halijakubali uraia wa nchi mbili.

“kinachowasumbua watu wengi ni maslahi wanayoyapa huku Ulaya”.

“Inakuwa ngumu kwa watanzania waliopo huku kuacha kazi zinazowalipa vizuri na kuja nchini”.

“Lakini kama suala la uraia wa nchi mbili litaruhusiwa, wengi watakuja”. Ameongeza Nditi.

Aidha, kinda huyo mwenye kipaji cha juu katika klabu ya Chelsea amesisitiza kuwa ifike wakati serikali iwafirie na kuukubali mfumo wa uraia wa nchi mbili kwani ni wajibu wa msingi kulisaidia taifa katika fani tofauti.

“Nchi yetu ina upungufu wa madaktari na wanamichezo bora, lakini wanashindwa kuja kusaidia Taifa”.

“Nasisitiza serikali ituruhusu na sisi tuje kuiokoa nchi yetu”. Amesema Nditi.

Nditi alizaliwa Zanzibar mwaka 1994 kabla ya kujiunga na timu ya Chelsea ya chini ya miaka 13 miaka kadhaa iliyopita baada ya kuhamia England na familia yake

0 comments:

Post a Comment