Jeshi la polisi mkoa wa Pwani linamshikilia Husna Iddi Kisoma (19) , mkazi wa Kisemvule Mkuranga mkoa wa Pwani kwa tuhuma za kumuua mumewe Jumane Mwalami (21) baada ya kumvuta sehemu za siri na kuzinyofoa kutokana na ugomvi uliosababishwa na wivu wa mapenzi.
Akizungumza na kipindi cha Maskani cha 100.5 Times Fm, kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Ulrich Matei ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku na kwamba kulikuwa na ugomvi kati ya wawili hao huku kijana huyo akimtuhumu mwanamke huyo kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume wengine.
Ameeleza kuwa wakati ugomvi unaendelea, mwanamke huyo alizishika sehemu za siri za mumewe na kuzivuta hadi kuzinyofoa.
Mwanaume huyo alipata maumivu makali na alikimbizwa hospitali ya Mkulanga ambapo alifariki.
Jeshi la polisi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo na tayari ameshafikishwa mahakamani akikabiliwa na kesi ya mauaji.
0 comments:
Post a Comment