Umati mkubwa wa watu
wamekusanyika mjini Vatican kushuhudia tukio la kihistoria ambapo
viongozi wawili wa zamani wa Kanisa Katoliki, Papa John Paul II na Papa
John XXIII wametangazwa watakatifu.
Ibada iliyoendeshwa kwa pamoja kati ya Papa
Francis na mtangulizi wake Papa Benedict XVI imeangaliwa na karibu
mahujaji milioni moja na wengine mamilioni ya watu kupitia matangazo ya
televisheni na redio.Karibu ujumbe wa wageni 100 wamehudhuria sherehe hiyo, wakiwemo kutoka koo za kifalme na wakuu wa nchi na serikali.
Hii ni mara ya kwanza kwa papa wawili kutangazwa kwa wakati mmoja kuwa watakatifu.
Waandishi wa habari wanasema hatua hii inachukuliwa kama njia ya kuziunganisha kambi mbili za wapenda mageuzi na wasiotaka mabadiliko ya sheria katika Kanisa Katoliki.
0 comments:
Post a Comment