Facebook

Sunday, 27 April 2014

Man City yaua,yakaribia kileleni................




LEO Yaya Toure ameiongoza Manchester City vyema kwenye Mechi yao ya Ugenini dhidi Crystal Palace na kuisaidia kushinda kwa magoli 2-0 na kuwakaribia Vinara Liverpool sasa wakiwa Pointi 3 nyuma yao na Mechi moja mkononi.

Toure ndie aliesuka goli la Kwanza alipotoa Krosi safi iliyounganishwa kwa Kichwa na Edin Dzeko na kutinga wavuni katika Dakika ya 4 tu.
Kwenye Dakika ya 43, Pasi ya Samir Nasri ilinaswa na Toure ambae aliupinda Mpira wavuni na kuandika goli la Pili.
Mechi inayofuata kwa Man City ni Jumamosi watakapokuwa Ugenini huko Goodison Park kucheza na Everton na wakishinda Siku hiyo watatwaa uongozi wa Ligi kwa kuwakamata kwa Pointi Liverpool, ambao hawachezi Siku hiyo, na kuwazidi kwa Ubora wa Magoli.

VIKOSI:
Crystal Palace: Speroni, Mariappa, Dann, Delaney, Ward, Jedinak, Ledley, Bolasie, Puncheon, Chamakh, Jerome
Akiba: Hennessey, Gabbidon, Parr, Dikgacoi, Ince, Gayle, Murray
Manchester City: Hart, Zabaleta, Kompany, Demichelis, Kolarov, Milner, Garcia, Toure, Nasri, Dzeko, Aguero
Akiba: Pantilimon, Lescott, Richards, Clichy, Fernandinho, Jovetic, Negredo.
REFA: Howard Webb


MECHI ZIZOBAKI:
Liverpool: Crystal Palace (Ugenini); Newcastle (Nyumbani)
Chelsea: Norwich (Nyumbani); Cardiff (Ugenini)
Man City: Everton (Ugenini); Aston Villa (Nyumbani); West Ham (Nyumbani)

Sunderland 4-0 Cardiff
Liverpool 0-2 Chelsea
Crystal Palace 0-2 Man City

Photo

0 comments:

Post a Comment