Facebook

Tuesday, 29 April 2014

Rick Ross a'spend $ 250,000 kuwanunulia zawadi Dj Khaled, Meek Mill na Wale..............


 
Rapa wa Miami mtu mzima Rick Ross ameingia gharama ya $250,000 kuwanunulia zawadi washkaji zake Dj Khaled, Meek Mill na Wale katika kusherehekea mafanikio ya Album yake mpya ya "MasterMind" aliyoiachia mwanzoni mwa mwezi March (12 March). Zawadi zenyewe ni Saa za mkononi sita, kwa maana hiyo kila mmoja amemzawadia saa mbili.
Moja ya saa hizo
Kwa mujibu wa TMZ wamereport kuwa mtu mzima Rozeey amedaka zawadi hizo kwenye moja ya sonara maarufu nchini Marekani inayofahamika kwa jina la "New York Jeweler Rafaello & Co.

Album ya Master Mind imekuwa namba moja kwenye chart ya Album bora zilizoachiwa mwaka huu, tangu kuachiwa mwezi March tarehe 12 ambapo project nzima imeingiza mauzo ya nakala 179,215 kwa week ya kwanza

0 comments:

Post a Comment