Sasa naona Nissan wameamua kumvuruga kichwa mshkaji wangu Emmanuel Mchunguzi, na
gari lao jipya lenye uwezo wa kujisafisha lenyewe, yaani hakuna kuosha
gari kabisa.
usishtuke sana bwana Emmanuel Mchunguzi, Nissan walaaaa, wanafanya yao tu, ila
licha ya kuwa ni gari kali, lakini siwezi kuliita gari linalojiosha
lenyewe (mtanisamehe Nissan) bali ni gari ninaloweza kusema halishiki
uchafu wa aina yoyote, na hata hiki kipande cha video kilichotolewa na
Nissan kinathibitisha hili.
Nissan wameanzisha rangi isiyoruhusu. vumbi, matope, uchafu wala maji
kubaki kweye body ya gari na kuiacha gari ikiwa ina ng'ara bila ya
kuiosha wala kuifuta.
Kwa mujibu wa Nissan rangi hiyo inazuia maji na mafuta pia, na ubunifu
huo ulifanikiwa kwa "kutengeneza tabaka la kinga ya hewa kati ya rangi
na mazingira".
Rangi hiyo inaitwa Ultra-Ever Dry na imetengenezwa na UltraTech International Inc.
Gari hili la majaribio linaonyesha upande wa kulia uliopakwa rangi hiyo na upande wa kushoto wenye rangi ya kawaida.
Angalia video hiyo hapa chini...
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kufahamu maendelea ya kasi yanayofanyika katika nyanja ya sayansi natechnolojia
0 comments:
Post a Comment