Facebook

Wednesday, 30 April 2014

Real Madrid yaivua rasmi Bayern Munich Ubingwa UEFA ....yawapiga 5-0.......

BAYERN Munich wamevuliwa ubingwa wa UEFA kwa kipigo cha mbwa mwizi baada ya kufungwa mabao 5-0 na Real Madrid katika mechi mbili za nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Mechi ya kwanza katika dimba la Santiago Bernabeu, Real Madrid walishinda bao 1-0 na leo hii katika nusu fainali ya pili kwenye uwanja wa Allianz Arena mjini Munich, kikosi cha Carlo Ancelotti kimeibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Real Madrid walitumia dakika 16 tu kufunga goli ambapo Luca Modric alichonga kona kutoka winga ya kulia na Sergio Ramos kujitwishwa mpira huo na kuuzamisha kimiani.

Dakika nne baadaye, beki huyo wa kati aliwamaliza Bayern baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu ndogo uliochongwa na Gareth Bale.
article-0-1D74992A00000578-72_634x423Baadaye Real Madrid walifanya shambulizi la kushitukiza ambapo Cristiano Ronaldo alifunga bao safi baada ya Bale kumpatia pasi murua.

article-0-1D74970700000578-13_634x445 
Bao hilo liliwafanya Real wahitimishe dakika 45 za kipindi cha kwanza kwa mabao 3-0.
Bao la dakika ya 90 la Cristiano Ronaldo kwa njia ya adhabu ndogo lilitia chumvi katika kidonda cha Bayern na kuvuliwa ubingwa kwa wastani wa mabao 5-0.

Kabla ya mechi hii, nyota wa zamani wa soka la Ujerumani, Stefan Effenberg alionesha wasiwasi wake kama falsafa ya Pep Guardiola itaisaidia Bayern Munich kutwaa ubingwa wa UEFA, wakati huu ambapo mchezaji muhimu Frank Ribery yupo katika kiwango cha chini.

Effenberg anaamini falsafa ya sasa ya Bayern ya kupiga pasi nyingi haikuweza kuwasaidia Bernabeu na alikuwa na wasiwasi katika mechi ya leo.

Kipigo cha mabao 4-0 kimethibitisha mawazo ya gwiji huyo wa soka la Ujerumani.
article-0-1D74811C00000578-501_634x452Tangu enzi za Zinedine Zidane, Luis Figo, Roberto Carlos na Raul, Real Madrid hawajacheza fainali na sasa wamefanikiwa kuelekea La Decima mjini Lisbon mwezi ujao.
Kabla ya mechi, watu walikuwa wanasema Real Madrid wanahitaji bao 1 zaidi au suluhu ili kuwashinda Bayern, lakini wameweza kushusha mvua kubwa ugenini.

Baada ya mechi hiyo, Gareth Bale amesema kipigo walichotoa leo hii ni sababu mojawapo ya yeye kujiunga na klabu kubwa duniani majira ya kiangazi mwaka jana.

“Ni matokoe mazuri mno kwetu. Nadhani tumejituma, tulitumia vizuri mbinu zetu na kucheza vizuri usiku huu, hivyo tulistahili ushindi”. Bale amezungumza na ITV.

“Walicheza mpira sana, waliacha nafasi za kushambuliwa kwa kushitukiza, nasisi tunapenda hivyo”.

“Tuna wachezaji wenye kasi na tunatumia nafasi kama hizo. Tulikuwa katika kiwango bora na tumefurahi kufika fainali”.

“Lakini kuna hatua nyingine mbele”.

“Kiukweli hii ndio sababu ya kwanini nilijiunga na Madrid. Ndio maana niliamua kuja kujiunga na klabu kubwa zaidi duniani”

“Lengo ni kushinda makombe na mechi kubwa. Tunatakiwa kushinda taji, tutakuwa na fainali ngumu kwa timu yoyote itakayopita kesho”.
article-2616240-1D74F53100000578-959_634x429Ronaldo baada ya kufunga mabao mawili usiku huu amevunja rekodi ya Lionel Messi kwa kufikisha mabao 16 katika msimu mmoja wa UEFA.


 

Real Madrid wamefuzu kwa mara ya kwanza fainali tangu walipofanya hivyo mwaka 2002 na kutwaa kombe na sasa wanatarajia kukutana na Chelsea au Atletico Madrid ambazo zitapambana kesho katika uwanja wa Stamford Bridge.
Mechi ya kwanza katika dimba la Vicente Calderon mjini Madrid, Chelsea walilazimisha suluhu ya bila kufungana, hivyo wanahitaji bao 1-0 ili kufuzu fainali

Related Posts:

  • FIFA YATANGAZA WATAKAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA Fifa imetangaza orodha ya majina 10 watakaowania tuzo ya mchezaji bora katika michuano ya Kombe la Dunia - 2014 Golden Ball. Wachezaji watatu wametoka Argentina, Angel Di Maria, Javier Mascherano na Lionel Messi. Maha… Read More
  • Refa wa fainali za Kombe la Dunia atajwa....!              Nicola Rizzoli amechaguliwa na Fifa kuwa mwamuzi katika mchezo wa fainali - Kombe la Dunia Brazil 2014 kati ya Ujerumani na Argentina.  &n… Read More
  • MAYWEATHER KUZICHAPA TENA NA MAIDANA Floyd Mayweather ametangaza kuwa atapanda ulingoni kupambana na Marcos Maidana, Septemba 3 mwaka huu mjini Las Vegas. Mayweather alimzidi Maidana katika mpambano uliozua utata mwezi Mei, na alisema kuwa atarudiana na … Read More
  • David Rudisha azidi kung'ara Olimpiki.   David Rudisha ameshinda mbio za mita 800 wanaume katika mbio za Diamond League za Scotland. Mara ya mwisho kuwa nchini Uingereza Rudisha alishinda medali ya dhahabu katika michuano ya Olimpiki ya London 2012. Mwa… Read More
  • LIVERPOOL NA BARCA WAKUBALIANA JUU YA SUAREZ   Liverpool wamefikia makubaliano ya kumuuza Luis Suarez kwenda Barcelona. Ada ya uhamisho inadhaniwa kuwa takriban pauni milioni 75. Suarez alijiunga na Liverpool mwaka 2011 akitokea Ajax, kwa pauni milioni 22.7. A… Read More

0 comments:

Post a Comment