Imedhihirika kuwa Mwanamuziki mweye asili ya Kongo Antoine Christophe Agbepa Mumba, maarufu kama Koffi Olomide hajachuja hata kidogo licha ya ukimya wake wa miaka mingi baada ya Mashabiki kubaki wakitaka zaidi katika shoo ya kukata na shoka aliyoifanya jijini Kampala Nchini Uganda.
Mwanamuziki huyu wa miondoko ya soukous, ambaye pia ni mcheza show, mtayarishaji Muziki na Mtunzi alikonga nyoyo za mashabiki baada ya kuwapa zaidi ya walichokuwa wakitarajia katika onyesho ambalo lilikua maalum kwa ajili ya kuchangisha fedha za kujenga maabara kwa ajili ya damu salama nchini Uganda iliyoandalia na klabu ya Rotary.
Kabla ya Koffi kupanda stejini alipanda mwanamuziki kutoka Canada, mlemavu wa Mikono ambaye alipiga ngoma kwa kutumia miguu yake huku akiwaacha maelfu wa mahabiki midomo wazi na kuufanya usiku ule kuwa usiku wa kihistoria Jijini Kampala.
0 comments:
Post a Comment