Serikali ya kijeshi ya Misri imetangaza kuwa chama cha Muslim Brotherhood ni kundi la kigaidi.
Uamuzi huo umetangazwa na Naibu Waziri Mkuu,Husam Muhammad Isa.Serikali imekilaumu chama hicho kwa shambulio la bomu lilofanywa Jumaane dhidi ya makao makuu ya polisi katika mji wa Mansoura, kaskazini ya Cairo ambalo liliuwa watu 13.
Imesema kuwa maandamano yote yatayofanywa na chama hicho ni kinyume cha sheria na mtu yeyote anayependekeza chama hicho atapewa adhabu.
Mwandishi mmoja mjini Cairo anasema Muslim Brotherhood imepigwa marufuku kwa miongo kadha na tangazo la sasa linachukua hatua zaidi - inamaanisha kuwa fedha na mali yote ya chama hicho sasa inaweza kutaifishwa.
0 comments:
Post a Comment