Facebook

Wednesday, 30 April 2014

Wachezaji Mbeya City wazuiwa kuhama timu........


WAKATI klabu kongwe za Simba, Yanga na Azam FC zikipiga hesabu za kuibomoa Mbeya City, Serikali imewaonya wachezaji hao kukihama kikosi hicho kinachofundishwa na Juma Mwambusi.

Zipo tetesi tofauti za wachezaji wa timu hiyo iliyomaliza ligi ikiwa katika nafasi ya tatu katika ligi kuwaniwa vikali na klabu hizo kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.


Akizungumza na Mwanaspoti, Mwenyekiti wa timu hiyo, Mussa Mapunda alisema Aprili 24, mwaka huu walipokea barua kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo iliyosainiwa na Naibu Waziri, Juma Nkamia ikiwasisitizia jambo hilo.


“Barua tuliyoipokea iliandikwa Aprili 15 kabla ya sisi kuipokea Aprili 24, ambayo imeelekeza kuendelea kuwapa matunzo mazuri wachezaji wetu wote bila ya kubagua kwa lengo la kukiboresha kikosi chetu ili msimu ujao kiimarike zaidi.


“Imetuonya kutowaruhusu wachezaji wetu kuwaachia kwenda klabu kubwa ambazo zenyewe hazina malengo na mpangilio wa kuziendeleza timu zao,”alisema Mapunda.


Wachezaji wanaotajwa kuwaniwa na klabu za Simba, Yanga na Azam FC ni Saad Kipanga, Hassan Mwasapili na Deus Kaseke.

0 comments:

Post a Comment