WAKICHEZA Ugenini huko Estadio de Mestalla, Vinara wa La Liga, Atletico Madrid wameifunga
Valencia goli 1-0 na kupaa kileleni wakiwa Pointi 6 mbele ya
Timu ya Pili, Real Madrid.
Atletico,ambaoJumatano wanasafiri
kwenda Stamford Bridge kurudiana na Chelsea kwenye Nusu Fainali ya UEFA , wanahitaji Pointi 6 tu katika Mechi zao 3 zilizobaki ili
wawe Mabingwa.
Bao la Atletico lilifungwa na Raul Garcia katika Dakika ya 43 kwa Kichwa alipounganisha Krosi ya Gabi.
Atletico walimaliza Mechi hii wakiwa Mtu
10 wakati Mchezaji wao Juanfran alipopewa Kadi Nyekundu kwa Rafu mbaya
katika Dakika za Majeruhi.
VIKOSI:
VALENCIA: Guaita; J.Pereira, R.Costa, Mathieu; Gaya; Fuego, Parejo; Barragan, Jonas, Piatti; Alcacer.
ATLETICO: Courtois; Juanfran, Miranda, Godin, Filipe Luis; Tiago, Gabi, Koke, Raul Garcia; David Villa, Diego Costa.
MSIMAMO-Timu za Juu:
NA | TIMU | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
1 | Atletico de Madrid | 35 | 28 | 4 | 3 | 75 | 22 | 53 | 88 |
2 | Real Madrid CF | 34 | 26 | 4 | 4 | 98 | 32 | 66 | 82 |
3 | FC Barcelona | 34 | 26 | 3 | 5 | 94 | 28 | 66 | 81 |
4 | Athletic de Bilbao | 34 | 18 | 8 | 8 | 59 | 37 | 22 | 62 |
0 comments:
Post a Comment