Nilipokuwa A-Level kipindi tuko likizo nilikuwa napenda sana kwenda kusoma masomo ya ziada(tuition) kwenye kituo kimoja kinaitwa Mapambano,nilikuwa natoka nyumbani Gongo la Mboto naelekea Mwenge kilipo kituo hicho.Nilipokuwa nikifika Ubungo ili nipande magari ya kwenda Mwenge nilikuwa namkuta Mchungaji akihubiri kuhusiana na siri za watu waabudu shetani.
Vivyo hivyo nikipita maeneo ya Ilala,Kariakoo,Mnazi Mmoja na Posta.Leo nimeamua kukuletea makala hiyo..
Kuna mtumishi kutoka Kenya yuko Dar es salaam anajulikana kama Mchungaji Joseph, amekuwa akizunguka vituo mbalimbali vya daladala akihubiri habari za Mungu na kusema mambo mbalimbali anayoyaita ni siri za shetani na kazi anazozifanya, Pia ni kwa jinsi gani watu wanachukuliwa misukule!
Mtumishi huyu alielezea aina ya nguo ambazo zimetengenezwa kuzimu na Mtu akivaa hizi zenye wanyama hawa, huonekana moja kwa moja kwenye ramani ya kuzimu
Alielezea kwamba aina ya nguo hizi mtu akivaa haishi miaka mingi, au kufa kifo kisicho cha kawaida
Pia alielezea huyo mnyama yupo anaishi baharini hivyo hiyo siyo picha tu!
Pia kulikua kuna kitambaa ambacho kilikua na alama mbalimbali ambazo anasema wanatumia wanaoabudu shetani au Freemasons. Na kusema pia wapo watu wanaosema ni wakristo wanatumia baadhi ya hizi alama hizi kwa kujua au kutokujua!
Pia lisema kuna wahubiri wawili ambao wanahubiri kwenye TV wanahubiri na kuponya kwa nguvu za giza ambapo wanatumia PETE zenye nguvu za giza . Ameliasa kanisa kuombea kazi ya Mungu kwa kumaanisha maana wapo watu wamejiingiza kanisani kama kondoo kumbe ni mbwa mwitu.
Alipokua akihitimisha mahubiri yake, alitaka watu watoe mafungu yao ya kumi na sadaka, pia aliwaombea wote waliokua na mahitaji mbalimbali.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua mambo mbalimbali yanayofanyika katika jamii yetu
nice
ReplyDelete