Facebook

Sunday, 27 April 2014

Rose Ndauka kuolewa hivi karibuni...........


MSANII maarufu wa sinema za Kibongo, Rose Ndauka amesema kuwa watu wasiwe na wasiwasi kwani kwa mipango ya Mungu atafunga ndoa na mzazi mwenzake Maliki Bandawe hivi karibuni.

“Si muda mrefu mambo yatakuwa mazuri tulikuwa tunaendelea kujuana, nadhani sasa tunafahamiana vizuri hivyo watu wasiwe na shaka, tutafunga ndoa soon,” alisema.


Rose ambaye hivi karibuni alihamasisha zoezi la usafi na kuungwa mkono na wasanii mbalimbali akiwamo Meya wa Ilala Jerry Slaa, alisema watu wasihofu kuhusu ndoa hiyo kwani ipo njiani.


“Hatujui labda kuchelewa kwetu kuna kitu Mungu amekiepusha, siku zote haraka haraka haina Baraka,” alisisitiza Ndauka ambaye amepanga kutembea Tanzania nzima kuwahamasisha wananchi kuzingatia usafi

0 comments:

Post a Comment