HALI
shwari sasa!. Mshambuliaji wa Manchester United, Mholanzi, Robin Van
Persie ameamua kuendelea kukaa katika klabu hiyo kufuatia kufukuzwa kwa
David Moyes.
Kilichomvutia zaidi nyota huyo ni
klabu hiyo ya Old Trafford kutaka kumleta Mholanzi mwenzake, Louis Van
Gaal kurithi mikoba ya ukocha mkuu.
Taarifa za kuaminika zinaeleza
kuwa Van Gaal tayari ameshakubali vipengele vya mkataba saa 48
zilizopita ili kuwa kocha wa kudumu wa Man united.
Sio siri kuwa Van Persie amekuwa
na mahusiano mazuri na kocha wake wa timu ya taifa na sasa anaona
itakuwa jambo zuri kukaa pamoja Old Trafford baada ya kumalizika kwa
fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Taarifa za ndani ni kuwa kocha
huyo wa Uholanzi na nahodha wake RVB wanatumia wakala mmoja, bwana Kees
Vos ambaye kwasasa yupo katika vikao vya makubaliano ya kazi mpya baina
ya Van Gaal na Man United.
Van Persie alikuwa akihusishwa
kuihama Man United majira ya kiangazi mwaka huu kwasababu klabu yake
imeshindwa kufanya vizuri kama ilivyokuwa katika msimu wake wa kwanza
ambao alibeba taji chini ya Sir Alex Ferguson.
Pia kulikuwa na hali ya kutoelewa
na bosi wake David Moyes kwa madai kuwa mbinu za ufundishaji za
Mscotish huyo zilikuwa haziendani na mfumo wa uchezaji wa Van Persie.
Lakini nahodha huyo wa zamani wa
Asernal ameamua kukaa Man United hata kama klabu inatarajia kusaka
mshambuliaji mwingine wa kati kwa sababu bosi wake anakuja.
0 comments:
Post a Comment