Facebook

Wednesday, 23 April 2014

Chelsea wamfukuzia Gabi,Cech na Terry waumia vibaya.............fuatilia hapa............


389319_heroa

BAADA ya suluhu pacha ya bila kufungana ( 0-0) na Chelsea, nahodha wa Atletioc Madrid, Gabi amekerwa na mbinu ya `kupaki basi` waliyotumia wapinzani wao katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali, ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Atletico wanaosifiwa kujilinda katika ligi ya Hispania, La Liga wamekutana na Chelsea ambayo ina uwezo mkubwa wa  `Kupaki basi` kwenye ligi ya England.
Katika nusu fainali hii ambayo haitasahaulika kwa Atletico, vinara hao wa La Liga  walimiliki mpira kwa asilima 62 na kupiga mashuti 26 golini, wakati Chelsea walipiga mashuti matano tu.
Matokoe ya leo yanaonekana kuwa mazuri kuelekea mechi ya marudiano darajani, ambapo washambiliaji wawili wa Chelsea Eden Hazard na Samuel Eto`o watarejea uwanjani.
Gabi amekiri kuwa matokeo ya leo yamewaacha katika hatari kubwa.
“Hatujaridhika, lakini mechi bado. Atletico walihitaji kushinda kutoka mwanzo wa mchezo hadi mwisho”.
“ Tulijua Chelsea wasingekubali kufungwa kirahisi na mwisho wa siku tumetoka kapa”. Gabi amewaambia waandishi wa habari.
Atletico hawajafungwa katika michuano ya kimataifa mwaka huu, lakini matokeo ya leo yamewafanya washindwe kupata ushindi kwa mara ya kwanza katika michuano ya ulaya msimu huu wa 2013/2014.
Katika mechi ya leo, Chelsea wamepatwa na majanga baada ya nahodha wake, John Terry  na mlinda mlango namba moja, Petr Cech kupata majeruhi.

article-2610536-1D457B4000000578-7_634x362 

Leo nusu fainali ya pili itashuhudiwa katika dimba la Santiago Bernabeu ambapo Real Madrid watawakaribisha mabingwa watetezi, Bayern Munich.
Hii inatazamiwa kuwa nusu fainali ya dunia kutokana na ukubwa wa klabu hizi mbili.

Related Posts:

  • Van Gaal: ''FIFA imetuonea'' Van Gaal akashifu FIFA kwa ratiba mbaya za mkondo wa pili Kocha wa Uholanzi Louis van Gaal amelishutumu shirikisho la soka duniani FIFA kwa "kufanya hila" kwa jinsi linavyopanga ratiba ya michuano ya Kombe la Dunia… Read More
  • Uholanzi kumenyana na Mexico Uholanzi kuvaana na Mexico mkondo wa pili Uholanzi ilimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye kundi B kufuatia ushindi wa mabao 2-0 katika mechi yao ya mwisho ya makundi. Mabao ya Uholanzi yaliyofungwa na Leroy Fern na… Read More
  • Brazil kuchuana na Chile raundi ya pili Brazil ilitamatisha mechi za kundi kwa kishindo iliilaza Cameroon 4-1 Neymar alifunga mara mbili katika mechi aliyokuwa mchezaji bora wak… Read More
  • Suarez apewa adhabu kali na FIFA STRAIKA wa Uruguay Luis Suarez amefungiwa Miezi Minne kutoshiriki chochote kwenye Soka baada ya kupatikana hatia ya kumuuma Meno Beki wa Italy Giorgio Chiellini. Straika huyo wa Liverpool pia amefungiwa Mechi 9 za Kimata… Read More
  • SUAREZ ADAIWA KUMNG'ATA MCHEZAJI TENA Picha za video zimeonesha mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez akimng'ata beki wa Italy Giorgio Chiellini. Mwamuzi hakuona kitendo hicho lakini huenda hatua zitachukuliwa baadaye. … Read More

0 comments:

Post a Comment