Facebook

Tuesday, 22 April 2014

Messi kuongezwa mkataba Barca ................fuatilia hapa...................


MESSI-HETITRIKI-16MACHI
























MARA baada ya Jana Lionel Messi kuisaidia Barcelona kutoka nyuma kwa Bao 1-0 na kufunga Bao la Pili na la ushindi walipoifunga Athletic Bilbao Bao 2-1 kwenye Mechi ya La Liga na kuifanya Barca ikamate Nafasi ya Pili Pointi 4 nyuma ya Atletico Madrid, Rais wa Klabu hiyo, Josep Bartomeu, amesisitiza Staa huyo atapewa Mkataba mpya ili kumbakiza Klabuni hapo.

Kumekuwa na minong’ono kuwa Mchezaji huyo atahama Nou Camp baada ya Msimu huu kuwa mgumu kwake na kukabiliwa na maumivu ya mara kwa mara lakini Josep Bartomeu amedai si haki kumlaumu kwa kushuka kiwango chake.
Josep Bartomeu amesema: “Messi ana Mkataba hadi 2018 lakini tunataka kuuboresha na uende sawa na hali ya sasa ya Soka. Watu hawamtendei haki kumlaumu Messi. Amiongoza Barca kwenye ushindi katika Miaka mingi sasa.”
Hivi sasa kumezagaa uvumi kuwa Manchester City, na hata PSG, wanawania kumnunua Mchezaji huyo ambae anadaiwa  kutofurahishwa na Neymar kulipwa zaidi yake ingawa hili halijathibitishwa.


Lionel Messi-Msimu huu:
-Mechi: 39
-Magoli:  41

Related Posts:

  • MADEGA "NILIMPITISHA OKWI ACHEZE SIMBA"Mwenyekiti wa zamani wa Yanga ambaye yupo kwenye Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Imani Madega Wilbert Molandi na Julieth Patrick MWENYEKITI wa zamani wa Yanga ambaye yupo … Read More
  • Who is Emmanuel Okwi.??? Katika nchi aliyozaliwa Sunday Manara "Computer", nchi aliyozaliwa Abdallah "King" Kibadeni,nchi aliyozaliwa Hamis Thobias "Gaga", nchi aliyozaliwa Method Mogella "Fundi" nchi aliyozaliwa Edibily Lunyamila, nchi aliyozaliwa … Read More
  • BIG BROTHER AFRICA YAAHIRISHWA 'KWA MUDA'   Uzinduzi wa kipindi cha 'Big Brother Africa' umeahirishwa kwa muda baada ya moto mkali kuzuka katika jengo linalotumika kama studio za kuendeshea kipindi hicho jijini Johannesburg. Kipindi hicho, kilichokuwa ki… Read More
  • Florentino Perez "SWEETY DADDY";Roho ya Florentino Perez ilivyomuingia Ed Woodward. Florentino Perez, Rais wa klabu tajiri duniani ya Real Madrid a.k.a Sweety Daddy, Tycoon katika ulimwengu wa soka. Mashabiki wa Real Madrid kuanzia viunga vyote vya mji wa Madrid, bara la Ulaya mpaka Asia, Africa kupitia ba… Read More
  • MAKALA:Busara za Kiimbila. ...........ASANTE "GENIUS" DI MARIA.............         Huwa nakumbuka sana wakati tunasoma shule zetu za "kayumba" na pengine hata za sekondari kwamba kulikuwa kuna kufaulu na kufeli, kuw… Read More

0 comments:

Post a Comment