Mwanaume aliyemuua kwa kumkata kichwa mpenzi wake amepatikana na hatia
ya mauaji nchini Uingereza
Aras Hussein alimkata kichwa mwanafunzi mwenye umri wa miaka 18 Reema
Ramzan nyumbani kwake katika mtaa wa Sheffield mwezi Juni kabla ya yeye
mwenyewe kujidunga kisu kifuani mwake.
Aras amehukumiwa kifungo cha maisha jela.
Hussein, alikiri kumuua mpenzi wake baada ya kuzozana ingawa awali
alikana madai ya mauaji.
Mwili wa Ramzan ulipatikana katika sehemu ya jikoni ya nyumba ya Hussein
tarehe nne mwezi Juni.
Polisi walipigiwa simu na mpita njia mmoja aliyemuona Hussein akitembea
uchi nje akiwa na damu katika mwili wake.
Madaktari walipojaribu kumsaidia kwa kumpa huduma ya dharura aliwauliza
kwa nini walikuwa wanataka kumsaidia wakati amemuua mtu nyumbani kwake.
Alipoulizwa kwa nini alifanya hivyo, akajibu kuwa hajui.
Mahakama ilisikia ambavyo msichana huyo alidungwa kisu kifuani na kisha
kukatwa kichwa chake.
Pia mikono yake ilikuwa na alama za kuonyesha kuwa alijaribu kujikinga
kutokana na kushambuliwa na mpenzi wake
Kiongozi wa mashitaka aliambia mahakama kuwa marehemu Ramzan bado
alikuwa hai wakati Aras alipoanza kumkata koo kwa kutumia nguvu.
Wakati kesi ilipokuwa inaendelea , mahakama iliambiwa na familia ya
Ramzan kuwa hawakupenda uhusiano kati ya wawili hao.
Siku ya kuuliwa kwake, alikuwa amekwenda nyumbani kwa Aras akiwa na Pasi
yake ya usafiri pamoja na kitita kikubwa cha pesa.
Chanzo
Friday, 18 April 2014
Inasikitisha:Msichana amchijna mchumba wake na kubaki na kichwa .....soma hapa....
Related Posts:
Aponea chupuchupu kwenye gurudumu la ndege.............fuatilia hapa kisa hiki........................ Karibu robo ya watu wote wanaosafiri wakiwa wamejificha katika gurudumu la ndege hufariki Mvulana mmoja mwenye umri wa miak… Read More
Majanga nchini Kenya; Al shabab watangaza kufanya shambulizi lingine.......fuatilia hapa....... Tishio la kigaidi lina kodolea macho taifa la Kenya baada ya kundi la kigaidi lililo na makao yake makuu nchini Somalia kuachia video nyingine kwenye mtandao wa Al-Kataib wakitishia kutekeleza mashambulizi nchini K… Read More
Wazazi waomba Boko Haram kuwa na huruma ,Nigeria.......soma hapa............ Jeshi limekosa kudhibiti kundi la Boko Haram licha ya vita vya mda mrefu dhidi ya kundi hilo Wazazi na jamaa w… Read More
Onyo la Marekani kwa Urusi ........soma hapa............... Joe Biden ameonya Urusi dhidi ya kuendelea kudhibiti mji wa Crimea Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden amesema sharti Urusi ik… Read More
'Tattoo' yamtia mashakani mtalii Sri Lanka................fuatilia hapa kisa hiki....................... Tatoo ya Naomi Michelle Coleman inaonyesha picha ya Budhaa ambaye ni Mungu wa waumini wa dini ya Budhaa. Mtal… Read More
0 comments:
Post a Comment