Friday, 18 April 2014
Mwiguli "asiyefanya kazi na asile".. Ukawa Kunyimwa Posho Bungeni.....fuatilia hapa..........
Ni Siku ya pili tangu Wajumbe wa Bunge la Katiba Kutoka Vyama vya Upinzanii wanaounda kitu kinachoitwa UKAWA wasusie Shughuli za Bunge la Katiba kwa Madai wamechoka Kutukana na Kuburuzwa kwenye Bunge hilo.
Hii leo Naibu waziri wa Fedha Mh.Mwigulu Nchemba ambaye kwa Sasa anakaimu Kuwa Waziri wa Fedha tangu Tarehe 10-04-2014 hadi 18-04-2014 kutokana na Waziri wa Fedha kusafiri Nchini Marekani Kikazi,amefuta Malipo ya wabunge waliosusia Mchakato wa Katiba.
Habari za Uhakika Kutoka hazina kinasema,Mwigulu Nchemba ameagiza Mabenki yote kurudisha hundi za Malipo ya Posho na {seating allowance} zilizopelekwa na Bunge jana tar.16-04-2014 ili ziwekwe kwenye akaunti binafsi za Wabunge ikiwa ni Malipo ya Mpaka tar.30-04-2014.
Mjomba mmoja ndani ya bunge hilo alisema fedha zote zinapitia Benki na wakati wanajiandikisha siku za Kwanza walitakiwa Kuandika namba zao za Benki na Malipo yote hupitia huko,hivyo kama ni fedha zinazuiliwa Benki.
Baadhi ya wabunge wa Upinzani wanaounda UKAWA toka jana walijua wameshasaini fedha hizo hivyo zitaingia kwenye account zao Binafsi. Mambo yamekuwa tofauti baada ya Naibu Waziri wa Fedha(Sera) Mh.Mwigulu kuagiza leo form zisainiwe upya leo na zitasainiwa pia tar 22 mpaka 25,Kwa madai ya "asiyefanya kazi na asile".
Mbali na hilo,Mh.Mwigulu amenukuliwa akisisitiza Rais kuwafuta wajumbe waliojitoa na badala yake awateue watu waliotayari kutunga katiba hata bure kuliko hawa wanaokutana vikao lukuki kupanga njama za kususia mchakato.
Aidha Mwigulu alisema fedha inayotumika ingeweza kulipwa Wazabuni wanaozidai halmshauri, wangeweza kulipa madeni ya walimu, au kuwapa mikopo watoto wa masikini waliofaulu ila hawajaenda vyuo kwa kukosa mikopo, au zingenunua madawa hosipitalini, au zingepeleka umeme, maji, vitabu au barabara lakini wamelipwa wajumbe badala ya kufanya kazi hiyo wanapanga njama ya kuhujumu mchakato usiendelee kwa kutafuta visingizio lukuki.
Bunge la Katiba linategemewa kuendelea Tar.22 Mwezi huu mara baada ya sikukuu za Pasaka Kupita na litaahirishwa tena Tar 25 mwezi huu kupisha Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata taarifa ya kila jambo linaloendelea katika Bunge la katiba mjini Dododma...
Related Posts:
Chenge akata rufaa asihojiwe Baraza la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kwa mara nyingine leo limeshindwa kumuhoji Mbunge wa Bariadi Magharibi kupitia CCM Andrew Chenge. Baraza hilo lim… Read More
BantuTz MAGAZETINI:-SOMA KILICHOANDIKWA KATIKA MAGAZETI YOTE YA LEO FEBRUARI 28 BantuTz MAGAZETINI:Ni miongoni mwa huduma bora kabisa tunazozitoa ili wewe mdau wa Bantu usipitwe na habari,stori au taarifa yoyote ile.Tunakuletea kila tunachokipata kwa wakati na muda muafaka.Soma kilichoandikwa katika k… Read More
Ndege ya Jeshi yaanguka na kuwaka moto uwanja wa ndege Mwanza, rubani anusurika! Taarifa kutoka Mwanza Airport ni kuwa kuna ndege ya Jeshi imelipuka na kuteketea. Rubani wa ndege hii, ndg Peter Augustino kafanikiwa kuruka kwa parachuti na kunusurika ingawa inadaiwa kavunjika mguu na kukimbizwa hosp… Read More
Mbunge John Komba afariki dunia Mbunge wa Mbinga Magharibi Mh. Kapteni John Komba amefariki Dunia leo saa 10 jioni katika Hosptali ya TMJ Mikocheni. Kwa Mujibu wa mtoto wa Marehemu Bw. Jerry Komba am… Read More
Dkt. Magufuli aongoza wananchi kwenye majaribio ya uzinduzi wa kivuko cha MV Dar es Salaam Leo Dkt.Magufuli amewaongoza wananchi wa Dsm kwenye majaribio ya uzinduzi wa Kivuko kipya Cha MV DAR ES SALAAM kitakachofanya safari zake kati ya Dsm na Bagamoyo, ambapo mamia ya wananchi walkiwana Waziri M… Read More
0 comments:
Post a Comment