Wednesday, 23 April 2014
Maige apinga serikali tatu,adai itakuwa maajabu ya dunia .......................fuatilia hapa.............
Mjumbe wa Bunge la Katiba, Almas Maige amesema endapo wajumbe wa Bunge hilo watapitisha muundo wa Serikali tatu, nchi itaingia katika kitabu cha maajabu ya dunia cha Guiness Book of Records.
“Hili litakuwa shirikisho la pekee hapa duniani lenye marais wengi katika nchi mbili, linaweza kuingia katika kitabu cha maajabu cha Guiness kwa kuwa na marais wengi katika nchi maskini sana,” alisema.
Mjumbe huyo alisema amejaribu kufuatilia hoja za wanaounga mkono muundo huo na kufananisha na nchi za Marekani na Nigeria, lakini akasema katika nchi hizo Rais wa nchi ni mmoja.
“Mimi nimejaribu kuwafuata wanaofananisha na Marekani na Nigeria, wameshindwa kusema katika nchi hizo mbili Rais ni mmoja tu hakuna wingi wa Rais kutokana na majimbo,” alisisitiza.
Katika hatua nyingine, mjumbe huyo aliwashangaa wajumbe wanaotokana na kundi la Ukawa kujigeuza kuwa wachunguzi wa kijinai kwa kuhoji uhalali wa saini ya muasisi wa Muungano, Abeid Aman Karume.
“Mimi nawashangaa sana wanasiasa hawa na wanasheria wa Ukawa wamejigeuza Forensic Expert (wachunguzi wa jinai). Mimi ningewaunga mkono kama wangeenda kuwauliza watoto wa marehemu,” alisema.
Aliongeza kusema: “Watoto wa marehemu wapo Zanzibar… Yupo Aman Karume aliyekuwa Rais wa Zanzibar na yuko Balozi Ali Karume na yuko pia mama Karume. Kwa nini hawawaulizi,” alihoji.
“Mimi ningefurahi sana kama wangeenda kuwauliza wanafamilia sahihi hii ni ya baba yenu? Au je, mheshimiwa mama hii ni sahihi ya mumeo? Wangekataa ndipo tungewaunga mkono,” alisisitiza.
Mjumbe huyo alisema kinyume chake, Ukawa wanavaa gamba la elimu ambayo hawana na vilevile hawajui maana na tafsiri sahihi iliyoandikwa miaka 50 iliyopita.
“Taaluma ya sasa ingeweza kugundua wino uliotumika una umri gani na kuondoa kero hiyo kama ni ya juzi au jana au kama imeghushiwa,” alisema mjumbe huyo na kuongeza kusema:
“Wataalamu wa Forensic (uchunguzi wa kijinai) wangeweza kugundua wino huo una miaka 50. Wanafanya kitu ambacho hawakijui na wanadhalilisha Watanzania.”
Mjumbe huyo alisema yeye anaunga mkono muundo wa Muungano wa Serikali mbili na kuwa Serikali tatu ni sawa na mtu kunywa sumu.
Related Posts:
Handaki la ajabu laonekana huko Iringa fuatilia hapa............ Umati wa watu waliofika katika eneo la kitanzini kuangalia handaki hilo mkuu wa Wilaya Ya Iringa mjioni Dkt Leticia Warioba akihojiana na mmiliki wa nyumba ambayo handaki hilo limeonekana Handaki lenyewe muonekano… Read More
Mwanachuo afia chumbani kwa hawara yake........... MSICHANA Atu Gabriel mwenye umri wa miaka 20, mwanafunzi wa Chuo cha Eden Hill kilichopo Kwamfipa wilayani Kibaha mkoani Pwani, amekutwa amekufa chumbani kwa mtu anayetajwa kuwa ni hawara yake, Hafidh Moh… Read More
Basi la Hood laungua vibaya Chalinze................ Zaidi ya Abiria 55 waliokuwa ndani ya Basi la kampuni ya Hood, wakisafiri kutoka Mbeya kwenda Arusha walinusurika kufa baada ya Basi hilo kushika moto na kuteketea kabisa katika kijiji cha Kilolele-Chalinze Mkoani … Read More
Binti achezea kichapo kwa wizi wa simu.............. Ni tukio lililotokea usiku wa jana (jumaapili) huko Nyumbani Park mkoani Morogoro, maarufu kama Samaki Samaki... mwanadada aliyedaiwa kuwa ni miongoni mwa wale wadada wanaofanya biashara ya kuuza mwili, ambapo hat… Read More
Ukawa mambo yapamaba moto watoa ratiba ya maandamano hii hapa....... Wana jamvi kuna mdau amenirushia ratiba ya ukawa mikutano na maandano nchi nzima kuanzia tarehe april 30-mei 4 kama ifuatavyo; dr slaa,mtatiro na prof safari watakua dodoma na pwani;maalim Seif Shariff Hamad na … Read More
0 comments:
Post a Comment