Wednesday, 23 April 2014
Waisalamu na Maaskofu waungana kutetea rasimu ya Warioba.......................fuatilia hapa............
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania imeungana na maaskofu mbalimbali kuwataka wajumbe wa Bunge la Katiba kuheshimu Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa kwa mujibu wa sheria na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Pia, taasisi hiyo imemtaka Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi kujiuzulu nafasi zake zote za uongozi kutokana na kauli waliyodai ya kichochezi, aliyoitoa katika Kanisa la Methodist, Jimbo la Dodoma kuwa ukipitishwa muundo wa serikali tatu, jeshi litachukua nchi kwa sababu itashindwa kuwalipa mishahara.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Msemaji wa Jumuiya na Taasisi hizo, Sheikh Rajab Katimba alilaani kauli kuhusu jeshi na kuwa makanisa yote yatafungwa na nchi itakosa amani kutokana na kupitisha muundo huo wa serikali.
Sheikh Katimba alisema Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa bungeni na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba imetokana na utafiti na uchambuzi wa maoni ya wananchi wa Tanzania Bara na Visiwani ili kuboresha Muungano kutatua kero zilizodumu kwa miaka 50 sasa.
Msimamo
Jumuiya hiyo iliweka wazi msimamo wake wa kutaka serikali tatu na kutaka maoni ya makundi mbalimbali ndani ya Bunge la Katiba kuheshimiwa.
Mjumbe wa Jumuiya hiyo, Sheikh Ramadhan Sanze pia alisema si ustaarabu kwa kundi moja kuhodhi mchakato kwa masilahi binafsi.
Alisema kukosoa maoni ya waasisi wa Taifa si dhambi kwa sababu wao hawakuwa Mungu kwamba hawakosei, badala yake alipendekeza watu waachwe wazungumze kwa utashi wa matakwa yao juu ya kile kilichowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
“Nchi hii haithamini mchango wa wataalamu, tumeona Tume ilivyofanya kazi nzuri, leo hii wanatukanwa hadharani, nawashangaa sana viongozi wa nchi hii,” alisema.
Sheikh Sanze alisema miiko na misingi waliyoiweka waasisi wa Taifa inavunjwa na viongozi wenyewe ambao leo wanasema waasisi wanatukanwa kwa kuwa wamependekeza serikali tatu badala ya mbili walizounda waasisi.
“Kulikuwa na utaratibu wa kubadilishana awamu za uongozi katika Serikali ya Muungano, awamu hii rais akitoka Tanzania Bara, ijayo atatoka Zanzibar; hii ndiyo misingi waliyoiweka waasisi, mbona leo haifuatwi? Huu ni unafiki...” alifafanua Sheikh Sanze.
Jumuiya hiyo imewataka wananchi wote kuendelea na mshikamano katika kutengeneza Katiba Mpya yenye maridhiano na itakayoondoa kero zilizodumu kwa zaidi ya miaka 50.
Related Posts:
Bosi wa EWURA Akutwa Amefariki Hotelini Meneja Biashara wa Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) amekutwa amekufa hotelini katika mazingira ya kutatanisha muda mfupi baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam akitoka Dodoma ambako alihojiwa na… Read More
Kimenukaa:Bosi wa Uda Kujieleza Bungeni Mgogoro wa uwekezaji katika Shirika la Usafirishaji Dar es Salama (Uda) umechukua sura mpya baada ya Bunge kuamua Mkurugenzi wa Simon Group inayoendesha shirika hilo, Robert Kisena ahojiwe na Kamati ya Kinga, Haki na… Read More
Madereva Wagomea na Kukisusa Kituo Kipya cha Daladala Ubungo Mwenge Wamiliki na madereva wanayofanya safari zake kati ya Ubungo na Mwenge jijini Dar leo wamegomea amri ya kutumia kituo kipya walichoamriwa na serikali kukitumia kilichopo nyuma ya jengo la Mawasiliano Tower, Ubungo jij… Read More
Mama Mzazi Amlipua Moto Mwanawe wa Kumzaa Dunia haina huruma! Mtoto Samwel Paulo (13), anayesoma darasa la nne Shule ya Msingi Amani wilayani Ilala, Dar, amelazwa wodi ya watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, akiendelea kuuguza majeraha yaliyotokana n… Read More
Kwa Kipindi Kirefu, MV Bukoba ilikuwa ‘Kaburi’ Lenye Kuelea Katika Ziwa Victoria RIPOTI ya Tume ya Jaji Robert Kisanga, iliyochunguza chanzo cha ajali ya mv Bukoba, inasema usiku wa kuamkia siku ya ajali, meli hiyo ilipakia abiria kati ya 750 na 800 pamoja na wafanyakazi 37. … Read More
0 comments:
Post a Comment