Wednesday, 23 April 2014
Paul Makonda awaita UKAWA watoto wa shetani na kagoma kufuta kauli.....................soma hapa..............................
Mjumbe wa Bunge la Katiba, Paul Makonda, jana aligoma kufuta kauli yake baada ya kuwaita viongozi wakuu wawili wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuwa ni watoto wa shetani.
Akichangia bungeni, Makonda alisema Mwenyekiti wa Ukawa, Freeman Mbowe, Mwenyekiti mwenza , Profesa Ibrahim Lipumba na mjumbe wa Ukawa, Ismail Jussa ni watoto wa shetani.
Shetani alikuja duniani kuiharibu dunia na kuteketeza kila kilichostahili kuungana… Lakini Yesu alikuja kuponya na kurekebisha kile kilichopotea,” alisema na kuongeza:
“Bahati mbaya sana shetani ni baba wa uongo, watoto wake ni mheshimiwa Jussa, watoto wake ni mheshimiwa Mbowe, watoto wake ni mheshimiwa Lipumba…Hawa ni watoto wa shetani.” Makonda aliwataka vijana nchi nzima wasikubali kupoteza muda wake kuambatana na viongozi hao katika matembezi yao, badala yake wajikite katika kufanya kazi za kiuchumi na kujiingizia kipato. Hata hivyo, baada ya kauli hiyo, mjumbe mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, aliomba mwongozo wa Mwenyekiti akisema Makonda alikuwa ametumia lugha ya kuudhi na isiyofaa.
“Huwezi kumwita mwanadamu mwenzako shetani… Aombe radhi na aondoe kauli hiyo mara moja” alisema na kumlaumu Mwenyekiti, Samuel Sitta kwa kuruhusu hali hiyo.
Sitta alisema “Ni kweli haipendezi kuitwa shetani nitamuomba mheshimiwa Paul Makonda aliangalie katika mazingira yetu na aweze kuyafuta hayo maneno”.
Hata hivyo, Makonda alisisitiza kuwa hawezi kufuta kauli yake wala kuomba radhi kwa sababu alikuwa amenukuu Biblia inayosema shetani ni baba wa uongo.
Baada ya kauli hiyo, Sitta alimtaka mjumbe aliyeomba mwongozo kurudi kwenye kanuni ili suala hilo liweze kupelekwa kamati ya maadili kama atataka kufanya hivyo.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata taarifa mbalimbali kuhusu mchakato wa katiba mpya
Related Posts:
Breaking News:Mwanza yachafuka,wamachinga wapambana na Jeshi la Polisi... Habari zilizotufikia hivi punde kutoka mkoani Mwanza ni kwamba kumetokea machafuko makubwa sana baada ya Jeshi la Polisi kupambana na Wamachinga. Ilikuwa ni mida ya asubuhi ambapo Jeshi la… Read More
Malawi waanza chokochoko ndege yao yaonekana Ileje MBUNGE wa Ileje, Aliko Kibona (CCM) ameomba Serikali ieleze juu ya ndege kutoka Malawi, ambayo imekuwa ikitia hofu wananchi wa Ileje, kwa kuzunguka angani kila mara. Mbunge huyo alisimama kutoa hoja hiyo baada ya… Read More
Soko la Karume lateketea kwa moto Usiku. Usiku wa kuamkia leo umekuwa mbaya kwa wafanya biashara wa Eneo la karume baada ya mabanda ya wamachanga katika eneo hilo kuteketea kwa moto , Chanzo cha moto huo kinadaiwa kuwa ni "Mama Ntilie" (ambao inase… Read More
Tanzania yawakumbatia wasomali.. Watoto hawa walikuwa miongoni mwa wale waliopokea vyeti vyao Serikali ya Tanzania imetoa vyeti vya uraia wa Tanzania kwa raia wa Somalia zaidi ya elfu mo… Read More
Hostel za wanafunzi zaungua moto vibaya Mbeya. Moto umetokea majira ya saa tano kasolo katika Chuo cha Mzumbe Tawi la Mbeya katika Vyumba vya kulala wanafunzi (hostel) ya Mputa zamani ilikuwa inafaamika kama block A. Watu wengine walikuwa ndani kama… Read More
0 comments:
Post a Comment