Van Gaal agrees to be next Manchester United manager

 Kocha  wa timu ya taifa ya Uholanzi,Louis Van Gaal hajasaini mkataba kama mbadala wa David Moyes kama kocha wa kudumu wa Manchester United lakini inasemekana ameshakubaliana na mabosi wa Manchester United ili kuja kuifundisha timu hiyo .

Louis Van Gaal amekubaliana kuja kusaini dili la miaka 3 baada ya kuwasiliana na   mmiliki wa Klabu ya Manchester United ambao ni familia ya Malcom Glazer ndani ya masaa 24 yaliyopita
Mdachi huyo anategemea kusaini mkataba usiopungua miaka 3 baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia ambayo itafanyika nchini Brazil mwez Juni.

Mkamu mwenyekiti wa Manchester United Ed Woodward na mmoja wa wanafamilia ya Glazer walikuwa kwenye makubaliano ya awali na Van Gaal huko Algarve anakoishi mdachi huyo.

Ingawa leo hii Manchester United wamekataa uvumi uliokuwa unaenea kwamba Van Gaal amesha saini mkataba na klabu hiyo.Lakini hawajakataa uwezekano wa Van Gaal kuja kufundisha klabu hiyo

 Vyombo mbalimbali vimeripoti kwamba wiki iliyopita Van Gaal aliongea na wawakilishi wa Man Utd na kusema kwamba anajisikia furaha kuja kuifundisha Manchester United baada ya kumalizika kwa fainali za kombe la dunia nchini Brazil akiwa na Timu ya taifa ya Uholanzi 'The Oranges'

Van Gaal anayefikisha miaka 63 ,Agosti tayari ameshaweka nia ya kuikacha timu ya taifa kwa ajili ya kuja kuinoa Man Utd kufuatia kutimuliwa kwa David Moyes baada ya viongozi wa klabu hiyo kukosa iman naye na sasa hivi wanataka kocha mwenye uzoefu, mafaniko makubwa na rekodi za kutosha kuipatia mafanikio klabu hiyo

Van Gaal  mwenye rekodi nzuri na ya kutisha barani Ulaya baada ya kufundisha vilabu vingi katika nchi tofauti tofauti na mwenye heshima kubwa katika soka la Ulaya na hivi sasa wengi wanatarajia makubwa kutoka kwake katika michuano ya kombe la dunia, mwezi July nchini Brazil

Vilevile Van Gaal ameshaweka wazi kwamba atamjumuisha mchezaji wa zamani wa Uholanzi, Newcastle United, Ajax na Barcelona, mdachi Patrick Kluivert katika benchi lake la ufundi

Kluivert Could Also Arrive As Assistant

 Mdachi huyo aliyewahi kuzifundisha Barcelona, Bayern Munich na Ajax Amsterdam ameshakutana mara 3 na viongozi wa Tottenham Hotspurs lakini amevutiwa zaidi kujiunga na Mashetani wekundu,na ameshawambia viongozi wa Tottenham kwamba hayuko tayari kufundisha klabu hiyo 

Vilevile amekuwa akiwindwa na mabosi wa Arsenal kutokana na mwenendo mbaya wa Arsene Wenger katika klabu lakini ameonesha nia ya kuja kuijenga upya Manchester United iliyofanya vibaya Msimu huu.

Imeandaliwa na....
                            Katemi Methsela (Blogger)
                                    0785 442 107

Source:Goal.com