Wednesday, 23 April 2014
Wabongo wamsusa Jack Cliff......................amwaga machozi kortini......................fuatilia hapa.........
HATIMAYE modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick ‘Jack Patrick’ amepandishwa kortini kwa mara ya kwanza huko Macau nchini China, Aprili 10, mwaka huu kwa kukutwa na madawa ya kulevya tumboni aina ya heroin kete 57 au kilo 1.1 yakiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 223 huku ishu kubwa kwa muda wote aliokuwa mahakamani ikiwa ni kuangua kilio kila wakati.
Jack alipandishwa kwenye korti hiyo ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu alipokamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’ Desemba mwaka jana akitokea Bongo kupitia Thailand na kuingia nchini humo. ILIKUWAJE? Kwa mujibu wa chanzo chetu makini kilichopo Macau, Jack alifikia hatua hiyo dakika 15 baada ya kupanda kizimbani na kukutana na nyuso za Wachina tu zikimwangilia
“Yeye alijua angekuta Wabongo au hata watu weusi wakimpa kampani, lakini matokeo yake alikutana na sura za Wachina tu,” kilisema chanzo chetu. Kikaendelea: “Unajua kwa kawaida mtu anapopanda kizimbani mara zote anafarijika sana endapo atawaona anaowafahamu, hasa ndugu zake ambao watafika kumtia moyo, sasa yeye hakulipata hilo.”
DAKIKA 10 ZATUMIKA KUMSOMEA MASHITAKA Kuna madai kwamba, msoma mashitaka wa mahakama hiyo alitumia dakika 10 kutokana na taratibu za kisheria za huko huku akitakiwa kusema ndiyo au hapana tu kabla keshi hiyo kupigwa kalenda hadi Mei 23, mwaka huu
KUNA MADAI ALIZOMEWA Chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, mbali na kukutana na upweke huo mahakamani, pia Jack alipata kisanga kingine pale baadhi ya raia wa nchi hiyo walipomzomea kwa sauti ya chini wakati akitoka kortini. Inadaiwa kuwa, kwa Wachina kumzomea au kumsema vibaya mtu aliyedakwa na madawa ya kulevya ni kawaida kwani hakuna biashara, inapigwa vita nchini humo kama ya unga wakiamini unaangamiza nguvu kazi ya kizazi kijacho. NDUGU WADAIWA KUMKATIA MAWASILIANO Habari nyingine kutoka chanzo chetu zilidai kwamba, kwa sasa Jack amebaki yeye na Mungu wake baada ya nduguze waishio Bongo kumkatia mawasiliano kwa kile walichodai kuwa kitendo alichokifanya kimeiaibisha familia nzima. “Unajua ndugu zake walikata mawasiliano kabisa? Nchi nzima au tuseme dunia nzima kilio ni jinsi vijana wanavyoharibika kwa madawa ya kulevya, sasa kule kubainika kwamba Jack alibeba unga tumboni kwenda kuuza kumeifanya familia kujisikia vibaya sana,” kiliongeza chanzo hicho kikiomba chondechonde kisitajwe gazetini.
KAMA ATARUDI BONGO SALAMA Habari zaidi zinadai kwamba modo huyo ambaye pia ni Miss Ilala No 3, 2005, aliwahi kumwambia mshirika wake mmoja akiwa mahabusu kwamba, kama atabahatika kurejea Bongo salama, atakwenda kupiga dua juu ya kaburi la mama yake ili amsimamie katika kumwondolea nuksi kama siyo mabalaa. Baba wa Jack anadaiwa kuishi nje ya nchi.
TUJIKUMBUSHE Jack alikamatwa Desemba 19, mwaka jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Macau nchini China akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guangdong Kusini mwa China ambako ilidaiwa ndiko alikokuwa anafikisha unga huo. Ilidaiwa kuwa miongoni mwa mambo yaliyochangia kukamatwa kwake ni kuonesha uso wenye uchovu, kuanza kuwa na hali mbaya ya mwili, kushindwa kujibu maswali vizuri na hati yake ya kusafiria, yaani ‘passport’ kukutwa imegongwa mihuri ya kuingia nchini humo kila mara jambo ambalo wakaguzi waliliona si la kawaida kwa msichana kama yeye.
Related Posts:
Salama aula DSTVSalama Jabir amepata shavu la kuonekana kwenye Tv tena akihost kipindi cha Tujuane ambacho kitakuwa kinaonekana kupitia televisheni ya Kenya. Katika kipindi hicho cha Tujuane Salama Jabir atakuwa akishirikiana na mtangazaji w… Read More
Taasisi ya Vicoba yawapatanisha Diamondi na Ali kiba.Kupitia programe yao ya FOCUS VICOBA itakayowezesha watanzania kupata mikopo online taasis hiyo imewakutanisha Plutnumz na Kiba na kuondoa tofauti zao kwa kutengeneza Tangazo la pamoja kuhamasisha uma kushiriki katika program… Read More
MISS TANZANIA MPYA NAYE UTATA MTUPU..... MISS Tanzania mpya wa 2014, Lilian Kamazima, amesema alihisi ushindi tangu alipoingia ka tika mashindano hayo, lakini alipokosa taji hakuhuzunika bali alikubali matokeo. Lakini zengwe jipya limeibuliwa jana na kuenezwa… Read More
Msanii wa muziki wa kuzazi kipya,Geez Mabovu afariki dunia muda mchache uliopita.Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini anayejulikana kwa jina la GEEZ MABOVU amefariki dunia. Ripota wa BantuTz akizungumza na dada wa marehemu anayetambulika kwa jina la Mammu amer… Read More
Ujumbe mzito wa Roma Mkatoliki baada ya kifo cha Geez Mabovu.Baada ya kuiona hii katuni, Roma Mkatoliki ameyaandika haya kutokana na kifo cha Geez Mabovu na stress. Tanzania inaomboleza kifo cha rapper Geez Mabovu ambae amefariki kwao Iringa akiwa hospitali jioni ya November 12 2014 ba… Read More
0 comments:
Post a Comment