Facebook

Monday, 14 April 2014

ATHARI YA KIFO CHA MAKABURI KWA ITIKADI KALI KENYA BADO HAIKO WAZI

Wakati wa mauaji yake, mhubiri wa Kiislamu wa Kenya Abubakar Shariff Ahmed aliheshimiwa kama mtu muhimu miongoni mwa wenye siasa kali, akichochea wasiwasi kwamba kifo chake kinaweza kuharibu jitihada za mjadala badala ya kuzuia itikadi kali kwa vijana katika mkoa wa Pwani.
  • Sheikh Abubakar Shariff Ahmed, anayejulikana kama Makaburi, amekaa chini ya bendera inayohusishwa na Uislamu wenye itikadi kali nyumbani kwake huko Mombasa tarehe 20 Februari 2014. [Ivan Liemann/AFP] Sheikh Abubakar Shariff Ahmed, anayejulikana kama Makaburi, amekaa chini ya bendera inayohusishwa na Uislamu wenye itikadi kali nyumbani kwake huko Mombasa tarehe 20 Februari 2014. [Ivan Liemann/AFP]
Ingawa Ahmed, anayejulikana kama Makaburi, amekuwa "kijana wa kazi" wa al-Shabaab nchini Kenya, kifo chake hakipaswi kusheherekewa, alisema Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Nelson Marwa.
Alisema kifo cha Makaburi kitawakatisha tamaa wanachama wa al-Shabaab kwa muda mrefu kama busara ya kupata mbadala haitapatikana, lakini kuondolewa kwake pekee sio mwisho wa itikadi kali na vurugu katika kipindi kifupi.
"Makaburi alikuwa sehemu ya mjadala ambao tumekuwa tukiufanya na viongozi wa dini, vijana, [asasi za kiraia] na jumuia kwa ujumla," Marwa aliiambia Sabahi. "Sina uhakika ni jinsi gani alijitolea kwa uaminifu kusababisha mjadala, lakini unaweza kuzuiwa kidogo."
Tuhuma kwamba serikali inaweza kuwa imehusika katika mauaji yake zinaweza pia kudhoofisha zaidi jitihada za amani za serikali katika mkoa wa Pwani, alisema.
"Lakini kwa mtazamo wa muda mrefu, [wafuasi wake] watakatishwa tamaa bila ya mtu wa kumuangalia kwa ajili ya kutiwa moyo na ufasaha wa kusema," aliongeza.
Ili kurejesha imani ya wananchi na kudhibiti uongezekaji wa vurugu, serikali itaendeleza mazungumzo ya kijamii, alisema.
Makaburi, aliyeuawa tarehe 1 Aprili na watu wenye silaha wasiyojulikana nje ya mahakama ya Shanzu huko Mombasa, alikuwa mtu mwenye mabishano aliyehusishwa na Masjid Shuhadaa (iliyokuwa Masjid Mussa) huko Mombasa, na alikuwa katika orodha ya watu wanaotafutwa kimataifa kwa kuunga mkono vikundi vya magaidi.
Alikuwa mshirika wa karibu wa Mwislamu mwenye itikadi kali Aboud Rogo Mohammed, ambaye aliuawa Agosti 2012 kwa kupigwa risasi akiwa katika gari. Mrithi wa Rogo Sheikh Ibrahim Ismail na wenzake watatu pia waliuawa kwa kupigwa risasi wakiwa katika gari mwezi Oktoba 2013, kulikochochea machafuko huko Mombasa.
Ingawa Makaburi hakuonekana kama mbadala wa moja kwa moja wa Rogo na Ismail, baada ya vifo vyao amekuwa kiongozi anayejulikana zaidi miongoni mwa watu wenye itikadi kali nchini Kenya.
Katika matukio yote matatu, polisi hawajawakamata washukiwa wowote na hakuna aliyeadhibiwa kwa vifo hivyo.
Marwa alisema uchunguzi ulikuwa ukiendelea ili kujua nani alihusika na vifo hivyo, akikataa madai kwamba serikali ilikuwa inahusika.
"Sio kazi ya serikali kuwaua washukiwa," alisema. "Hatuhusiki katika mauaji yaliyopita na ninaamini kwa dhati kwamba hatuhusiki katika kifo cha Makaburi."

Kuongezeka kwa itikadi kali ya Makaburi kwa muda

Mkurugenzi wa Polis wa Akiba na Polisi Jamii wa Kenya Aggrey Adoli, ambaye alifanya kazi kama mkuu wa polisi wa mkoa wa Pwani hadi Februari, alisema Makaburi hakuwa na ustadi wa kuzungumza na kipaji kama cha Rogo lakini alikuwa maarufu baada ya kifo cha Rogo.
Kabla ya kifo cha Rogo, Makaburi alionekana kama mkimya, mtaratibu wa kuongea na mwenye aibu sana kuweza kufikiriwa kuwa mbadala, Adoli aliiambia Sabahi.
"Mtindo wa hamaki na majibizano wa Rogo wakati wa kuhubiri, ibada na mihadhara ni tofauti sana na aina ya ushwari na utulivu wa Makaburi," alisema. "Lakini katika uwasilishaji na mwenendo wote wawili walikuwa na uwezo wa kuwapoteza na kuwaingiza vijana katika itikadi kali."
Wakati wa kifo chake, wafuasi waliona mawazo ya Makaburi ya kuwa mpole na asiyetaka kupambana kama wema wa kusambaza itikadi kali, alisema Adoli.
Makaburi pia alikuwa akiheshimiwa na wanajihadi kwa sababu ya mfungamano wake na al-Qaeda huko Yemen, kama alivyoripotiwa kusafiri kwenda huko mara kwa mara na kuishi huko kati ya mwaka 1980 na 1995.
"Kitu ambacho hakina uhakika ni kwamba katika kurudi kwake alianzisha mawazo ya ajabu wakati ambapo itikadi kali ilikuwa bado ni jambo la kushangaza nchini Kenya," alisema.
"Kama utawalinganisha wawili hao, Makaburi alikuwa na uhusiano wa karibu na Yemen ambako alishirikiana na watendaji wa al-Qaeda na pia alifundishwa kutumia bunduki mbalimbali," alisema Adoli, akielezea jinsi Makaburi alivyokuwa muhimu kwa mtandao wa wenye itikadi kali huko Mombasa hata wakati Rogo alipokuwa hai.
"Tulipokuwa tukichunguza shughuli zake mwaka 2010 Makaburi alikuwa akifanya kazi kwa siri," alisema, akiongeza kwamba mamlaka zisingeweza kukusanya ushahidi wa kutosha wakati huo ili kumshtaki.
Mwaka 2012, wakati polisi walipomhusisha na uandikishaji wa al-Shabaab nchini Kenya, Adoli alisema waligundua njia yake ya ufanyaji kazi imebadilika.
Baada ya kifo cha Rogo, Makaburi alihama kutoka shughuli za kutoonekana wazi hadi kuchukua wajibu wa uongozi unaoonekana na kuwa muongeaji zaidi na wazi kuhusu mawazo yake.
Makaburi aliondoa wasiwasi kuhusu utii wake kwa al-Shabaab wakati alipoelezea shambulio la maduka makuu ya Westgate huko Nairobi kama "ni la haki kwa asilimia 100".
"Tulishangazwa kidogo kwamba sasa alikuwa akiunga mkono vurugu hadharani, hata katika vyombo vya habari," Adoli alisema akielezea kubadilika kwa tabia ya Makaburi.
"Kuna watu wengine wanne au sita tuliokuwa tukiwafikiria katika vita ya ugaidi, lakini hakuna hata mmoja anayeweza kumbadili yeye kwa siku zijazo," alisema. "Makaburi alikuwa ndiye mtu wetu mkuu na kifo chake, bila kujali jinsi kilivyomkuta ni hatua nzuri katika vita ya ugaidi."

Kuwaua maulamaa kutasababisha msimamo mkali kwa vijana

Mchambuzi wa masuala ya usalama na mstaafu wa Jeshi la Kenya Kanali Daud Sheikh Ahmed pia alisema itakuwa vigumu kubadili ushawishi wa Makaburi na uhusiano wake katika siku zijazo.
"Kwa hivyo, Makaburi aliendelea pale alipoishia Rogo," Ahmed aliiambia Sabahi.
"[Pamoja na imani] kwamba alikuwa ni mtu aliyewekewa alama na angeweza kuuawa kwa njia yoyote, Makaburi alijitokeza hadharani," alisema. "Hata al-Shabaab huko Somalia hawawezi kufanya shughuli zao hadharani kama alivyofanya Makaburi. Hii inamtofautisha na kumpa msimamo mkali wa kumtofautisha."
Kwa hivyo, kifo cha Makaburi ni pigo kubwa kwa wenye itikadi kali na picha ya jumla ya al-Shabaab, alisema Ahmed, akiongeza kwamba kundi hilo litaonyesha ugumu kumpata Mkenya mwingine wa kuchukua nafasi zao.
"Kupitia Makaburi, al-Shabaab ilitaka kufuta madai kwamba kundi hilo [limeundwa] na Wasomali na linapigana kwa ajili ya Somalia tu," alisema.
Umuhimu wa hotuba za Makaburi katika miaka michache iliyopita ulikuwa ndiyo hasa kilichomfanya aungwe mkono na wafuasi wa Rogo na watu wengine kama hawa.
Hata hivyo, Seneta wa Kaunti ya Mombasa Hassan Omar Hassan alionya kwamba kama serikali itapatikana kuhusika na mauaji ya Rogo, Ismail na Makaburi, itachochea usemaji wa al-Shabaab na uandikishaji.
"Wote waliouawa wangeweza kuwaunga mkono al-Shabaab hadharani au makundi mengine ya ugaidi, lakini kuwaua badala ya kuwakamata na kuwashtaki kunaweza kuwa uhamasishaji wa kutosha kuwavutia Waislamu wenye msimamo wa kati ambao wamekuwa wakipingana na vurugu zinazosababishwa na al-Shabaab," Hassan aliiambia Sabahi.
"Mauaji haya yanatupatia viongozi wakati mgumu wa kupitia kwa watu wetu [na kuhakikisha kwamba wana] endeleza utulivu na kuheshimu sheria za nchi," alisema. "Tunaendeleza mazungumzo hayo kama suluhisho la vurugu hizi zinazoendelea. Itachukua muda zaidi kuliko serikali inavyotarajia lakini mauaji ya kutumia nguvu yanapunguza jitihada za mazungumzo."

         Imeandaliwa na Emmanuel Elias Masanja

0 comments:

Post a Comment