Msanii na mmiliki wa kampuni ya Unity Entertainment, Ambwene Yesaya
'AY' ameweka wazi nia yake ya kufunga ndoa kimya kimya wakati
utakapowadia.
AY alimweleza mtangazaji Salama Jabir wa kipindi cha 'Mkasi'
kinachorushwa na kituo cha televisheni cha EATV kwamba kuoa au kuolewa
si jambo la kukurupuka, linahitaji utayari hivyo atakapokuwa teyari
atafanya hivyo kama vitabu vya Mungu vinavyoeleza japo alidai kuwa watu
wanaweza kujua kama ameoa siku moja baada ya harusi yake.
"Naamini kila jambo lina wakati na wakati unapowadia litatimia tu. Kuoa
si jambo la kuiga kwa kuwa fulani ameoa leo na mimi nikaoe kesho au
keshokutwa, kuoa ni mpango na mpango utakapokamilika nitaoa ingawa watu
wengi mtajua siku moja baada (mimi) ya kuoa," alisema.
Kuhusu East Coast Team, AY alisema: "ECT halikuwa kundi la muziki kama
ambavyo watu walikuwa wakielewa bali tulikuwa tukiishi kama wanafamilia
hivyo ilipotokea mmoja wetu anafanya wimbo tulikuwa tukishiriki.
Mfano wimbo kama 'Komaa Nao', 'Ama Zangu Ama Zao', ni nyimbo za GK
lakini sisi tulikuwa tukishiriki hivyo hazikuwa nyimbo za kundi.
Lakini pia baada ya mimi kutangaza nimeondoka East Coast watu
walikuwa wakidhani kwamba huenda tukikutana na GK hata tusingeweza
kusalimiana, haikuwa hivyo kwakuwa sisi tulikuwa tunaishi kama familia
hivyo tuliendelea kuwasiliana na kutembeleana kama kawaida."
0 comments:
Post a Comment