Tuesday, 22 April 2014
Baby Madaha ajibu mapigo Kwa Steve Nyerere ........fuatilia hapa mapigo hayo............
VITA ni vita! Mwanadada shosti anayesukuma maisha kupitia filamu na muziki Bongo, Baby Joseph Madaha amesema anamshangaa Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ kwa kauli aliyoitoa dhidi yake kuwa hayupo sehemu yoyote ile.
Akifafanua kuhusiana na kauli hiyo aliyoitoa mwenyekiti huyo wiki iliyopita, Baby alijibu mapigo kuwa kiongozi huyo alipotosha umma kwani yeye ni memba halali wa Bongo Movie Unity.
“Steve anasema hajui nipo wapi, hivi ni kweli mwenyekiti hawajui watu waliokuwa na kadi ya uanachama? Mimi nipo kotekote, nipo Bongo Movie, nipo hata Bongo Fleva, kama akitaka kadi aseme nimwoneshe, sionekani sana kwani muda mwingi nakuwa Kenya,” alisema Baby Madaha, alipotafutwa Steve, hakuwa tayari kufafanua ishu hiyo.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari mbalimbali zinazowahusu wasanii
Related Posts:
Kilichosemwa na Polisi wa Kenya jinsi gari la Freeman Mbowe lilivyokamatwa..... Gari la kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni ambae pia ni mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe limekamatwa ambapo baadhi ya vichwa vya habari vilisema ni kutokana na kuhisiwa kut… Read More
Mlela akana kutumia madawa ya kulevya !!!!!!.. NYOTA wa filamu za Kibongo, Yusuph Mlela amedaiwa kugeuka teja (mbwia madawa ya kulevya) hali inayomsababishia ashindwe kujichanganya na wasanii wenzake katika shughuli mbalimbali.Kikizungumza na Amani juzikati, chanzo … Read More
Unakijua alichokisema Wolper kuhusiana na sakata la serikali mbili au tatu ????...... MWIGIZAJI staa Bongo, Jacqueline Wolper ameifungukia rasimu ya katiba mpya ambayo ipo bungeni kujadiliwa kwa sasa akisema yeye matakwa yake ni kuwepo kwa serikali mbili na si tatu wala ya mkataba. Wolper alisema ana… Read More
Tuzo za Diamond zampagawisha Wema....fuatilia hapa ujue alichokisema... Kila msichana hivi sasa anandoto za kuwa kama WemaSepetu hivi sasa, kwa kuweza kujivunia mafanikio ya mpenzi wake Diamond Platnumz, baada ya kuandika historia katika Game hili la muziki wa Bongo Fleva, kwa kuchukua… Read More
Kumbe Diamond alitoa chozi alipokuwa anarekodi ngoma ya "Kipi Sijasikia" ya Prof J...... Profesa J amesema Diamond Platnumz, alilia machozi wakati anafanya chorus ya wimbo wake ‘Kipi Sijasikia’Rapper huyo alikiambia kipindi cha Sunrise cha Times FM kuwa wakati Diamond anarekodi chorus hiyo yeye na Majani wali… Read More
0 comments:
Post a Comment