Facebook

Friday, 18 April 2014

Barca Majanga....Alba na Neymar Nje wiki nne.......soma hapa....

388904_heroa
 Mshambuliaji wao raia wa Brazil, Neymar ataa nje ya uwanja wa wiki nne, wakati naye beki Jordi Alba atakaa muda kama huo baada ya wote kupata majeruhi.
Klabu ya Barcelona imethibitisha kuwa Neymar alipata majeruhi ya mguu jana katika mchezo wa fainali ya kombe la Mfalme dhidi ya Real Madrid.
Kinda huyo mwenye miaka 21 alishindwa kuisaidia Barca kuepukana na kipigo cha mabao 2-1, huku Mbrazil huyo akikosa nafasi ya wazi dakika za lala salama.
Neymar atakosa mechi zijazo dhidi ya Athletic Bilbao, Villarreal, Getafe na Elche.
Hata hivyo klabu ya Barca ina matumaini kuwa nyota wake huyo anaweza kurudi katika mechi ya mwisho dhidi ya Atletico Madrid.
Taarifa ya klabu ya Barcelona imesema;”Mchezaji huyu aliumia jana katika mguu wake wa kushoto na anahitaji muda maalumu wa matibabu. Makadirio ya kurudi uwanjani ni wiki nne”.
Naye Jordi Alba alitolewa baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza katika mechi ya jana na taarifa zinaeleza kuwa beki huyo wa kushoto aliumia nyama za paja za mguu wake wa kulia.
Beki huyo wa zamani wa Valencia anaweza kukaa nje ya uwanja kwa wiki tatu hadi nne

Related Posts:

  • Rais Kikwete akagua kituo cha Michezo cha Kidongo Chekundu kinachojengwa na Klabu ya Sunderland,  Rais Jakaya Mrisho kikwete akitambulishwa na Mkurugenzi wa kampuni ya umeme ya Symbion Bw. Paul Hicks kwa kocha wa vija na kutoka Uingereza anayetambuliw3a na FIFA ambaye atakuwa mkufunzi Mkuu katika kituo hicho wa… Read More
  • Costa na Gabriel washtakiwa na FA.Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa ameshtakiwa kwa madai ya kutaka kuzua ghasia ambayo hayakuonekana na maafisa wa mechi hiyo lakini ambayo yalinaswa katika ukanda wa video. Mshambuliaji huyo alihusishwa katika kisa na beki … Read More
  • Van Gaal aimwagia sifa timu yake.Meneja wa Klabu ya Manchester United Louis van Gaal ambaye baada ya Ushindi wa jana mabao 3-2 dhidi ya Southampton sasa amesema kikosi chake kina uwezo wa kuchukua ubingwa wa Ligi ya England katika msimu huu wa ligi. Ushindi … Read More
  • YANGA YATUMA SALAMU MSIMBAZILigi Kuu ya Tanzania Bara imeendelea leo kwa kushuhudia viwanja vinne vikiwaka moto, ambapo katika uwanja wa Taifa Dar es salaam, mabingwa watetezi Yanga wamepata ushindi wa tatu mfululizo kwa kuichapa JKT Ruvu mabao 4-1. Mab… Read More
  • Ozil:Msituhukumu msimu bado haujaisha.  "Muda mwingine mambo hayaendi kama mlivyopanga, tumeharibu mechi mbili za karibuni, sasa tunajipanga kutofanya makosa, msituhukumu bado msimu ni mchanga na ni mapema mno kupoteza imani na timu"… Read More

0 comments:

Post a Comment