MENEJA
wa Muda wa Manchester United, Ryan Giggs, Leo hii ameongea na
Wanahabari kwenye Kituo cha Mazoezi cha Klabu hiyo na kutamka kuwa Siku
aliyoteuliwa Meneja ilikuwa ni Siku ya Fahari kubwa katika Maisha yake.
Giggs, mwenye Miaka 40, atakuwa Meneja
wa Man United kwa Mechi 4 zilizobakia kwenye Msimu huu na ameshika
wadhifa huu baada ya kufukuzwa David Moyes Jumanne iliyopita.
Akiongea huku akionyesha furaha na
kukiri kuwa anataka Man United ifanikiwe kucheza EUROPA LIGI Msimu ujao,
Giggs, Mchezaji mwenye mafanikio makubwa kwenye Klabu ya Man United,
alisema: “Ninasikia fahari, ninafuraha na kidogo nasikia wasiwasi!”
Giggs pia alidokeza mara baada ya
kuteuliwa Meneja, Simu yake ya kwanza ilikuwa kwa Meneja wa zamani wa
Man United, Sir Alex Ferguson, na alisema: “Nilitaka ushauri na nilitaka
nijue nini nitegemee.”
Pia Giggs alisema kuwa alipoanza kazi yake mpya Wachezaji wote walikuwa na ari mpya na furaha kubwa.
Ametamka: “Mkazo kwangu ni Mechi na
Norwich na zile 3 zilizobaki. Naingojea kwa hamu Jumamosi. Najua Old
Trafford itazizima na najua Mashabiki watatupa sapoti kubwa.”
Pia alifafanua kuhusu staili ya Uchezaji
wa Timu yake ya kucheza Soka safi la kushambulia kwa kusema: “Ni
Falsafa yangu na ni falsafa ya Manchester United!”
Awali Gigg s, akiongea na MUTV, Kituo cha
TV cha Man United, alisema: “Huu ni wakati ninaosikia fahari kubwa
kupita wakati wowote maishani mwangu. Nimeisapoti Manchester United
maisha yangu yote, nimekuwa sehemu ya Klabu hii tangu nikiwa na Miaka
13!”
Giggs ameichezea Man United mara 962,
ikiwa ni Rekodi, na kwenye kazi yake hii atasaidiwa na Wenzake alioanza
nao kucheza nao Man United, Phil Neville, Nicky Butt na Paul Scholes.
Mechi ya Kwanza ambayo Giggs atasimamia
kama Meneja ni Jumamosi Uwanja wa Old Trafford dhidi ya Norwich City
kwenye Ligi Kuu England.
Video inayoonyesha Ryan Giggs alipokutana na waandishi wa habari leo kwenye mkutano wake wa kwanza kama kocha wa Manchester United ...angalia....katemimethsela.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment