Facebook

Friday, 25 April 2014

Carlo Anceloti aukubuli mfumo wa Guardiola Bayern Munich..............



394673_heroa

KOCHA wa Real Madrid, raia wa Italia, Carlo Ancelotti ameutetea mfumo aliotumia Pep Guardiola wakati klabu yake ilipopambana na Bayern Munich katikati ya wiki na kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Guardiola raia wa Hispania alikosolewa kwa mfumo wake aliotumia jumatano ya wiki hii ambapo timu yake ilifurahia kumiliki mpira, lakini iliambulia kichapo.
Kocha huyo wa zamani wa FC Barcelona tayari ameshabeba taji la Bundesliga msimu huu, lakini Ancelotti amesema ana mfumo mzuri na sasa hawezi kuzungumza lolote zaidi ya kuangalia mchezo wa kesho wa La Liga dhidi ya Osasuna
“Napenda mfumo wa Guardiola. Alileta mfumo mpya katika mpira. Ana aina ya mpira wake”. Ancelotti amewaambiwa waandishi.
“Nampenda sana mfumo wa Pep, ameleta aina yake ya mpira, alitumia akiwa Barca na sasa anautekeleza akiwa Bayern, japokuwa kuna ugumu kwake”.
“Bayern imefanikiwa na kocha wake. Pep anafanya kazi nzuri. Lakini bado hatujaanza kufikiria mechi ya Munich kwasababu mechi ya kesho ni muhimu kwetu”.
Ancelotti amekuwa akihusishwa na taarifa za yeye kujiunga na Manchester United kufuatia kutimuliwa kwa David Moyes, lakini kocha huyo wa zamani wa Chelsea amesema hafikirii kuondoka Santiago Bernaberu kwa sasa.
“Kila mwaka haya yanatokea na nazungumza kitu kile kile. Nina furaha kuwepo hapa”.
“Najiona mwenye bahati kuwa na moja ya klabu bora zaidi duniani. Nawaheshimu Man United na kile kilichomtokea Moyes, lakini nipo hapa”. Alisema Ancelotti.
Ancelotti ataiongoza Madrid Allianz Arena jumanne ya wiki ijayo, baada ya mechi ya kesho ya La Liga dhidi ya Osasuna.
Ataingia katika mechi hiyo nusu fainali ya pili ya UEFA akiwa na faida ya ushindi wa bao 1-0 na atahitaji kuulinda ushindi huo ili kukutana nna Chelsea au Atletico katika mchezo wa fainali mei 24 mwaka huu mjini Lisbon nchini Ureno.

0 comments:

Post a Comment