Facebook

Monday, 14 April 2014

IDADI YA WATU WALIOKUFA KWENYE MILIPUKO ABUJA YAONGEZEKA

Zaidi ya watu 70 wameuawa katika milipuko miwili ambayo imetokea katika kituo cha mabasi mjini Abuja, Nigeria.
 Milipuko hiyo ilitokea wakati abiria wakiwa katika harakati za kupanda mabasi na teksi wakienda maofisini katikati ya mji wa Abuja.
Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema miili ya watu imetapakaa katika eneo la tukio.
Kundi la wapiganaji wa Kiislam la Boko Haram ambalo limehusishwa na mashambulio ya awali nchini humo pia limehusishwa na milipuko hiyo.
Hata hivyo, mashambulio mengi ya kundi hilo yamekuwa yakifanyika kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo.
Abbas Idris, mkuu wa Shirika la Misaada la Nigeria,anasema wamethibitisha watu 71 kuuawa na wengine 124 kujeruhiwa.
Askari wakiwa wamesimama mbele ya mabasi yaliyounguzwa baada ya mlipuko mjini Abuja,Nigeria
Msemaji wa polisi Frank Mba ametoa takwimu kama hizo, akiongeza kuwa mabasi 16 ya kifahari na mabasi madogo 24 yameharibiwa.



Endelea kufuatilia hapahapa habari zaidi na kwa muda muafaka
  katemimethsela.blogspot.com


0 comments:

Post a Comment