Facebook

Tuesday, 15 April 2014

UBUNIFU NA MITINDO

Ni matumaini yangu kwamba kupitia nakala hii utaweza kufahamu kwa undani maana na umuhimu Wa ubunifu katika mavazi "dress on codes".

Suala la kuonekana nadhifu na mtanashati ni juhudi na uwezo wa ubunifu juu ya mavazi ukihusianisha na muonekano Wa mwili wako.
Kwani unaweza kuwa na pesa za kutosha, ukavaa vitu vya gharama lakini usiwe na muonekano mzuri mbele ya jamii.


VITU VYA KUZINGATIA :
1.Jua mwili wako yaani kama ni mfupi,mrefu,mnene au mwembamba.

2. Jua rangi ya ngozi yako kisha jaribu kuambatanisha na aina za rangi za mawazi zitakazoendana na ngozi yako
- usipende kuvaa nguo zenye rangi ya mng'ao hasa wakati Wa mchana.

3. Tambua aina ya mavazi unayopendelea. Husianisha na aina ya jamii inayokuzunguka inachukuliaje aina hiyo ya mavazi (mf. Unapokua na rika la vijana au rika la watu wazima).
- tambua nyakati za kuvaa kila aina vazi.

VIFUATAVYO HUONGEZA MUONEKANO NA MVUTO: 1. Miwani.
Unapovaa miwani hasa unapotaka kupiga picha huongeza mvuto na kukupa muonekano mzuri. Hii imefanyiwa utafiti na "designers" mbalimbali duniani.
Njia hii hutumika na watu wengi maarufu na hata wasiomaarufu. Mfano: Msanii Mkubwa Tanzania Naseeb haroub yaani DIAMOND PLATNUMZ. hii humpatia muonekano mzuri katika picha zake.

2. MATUMIZI YA KOFIA.:

Mara nyingi kofia hutumika kwa kazi ya kuzuia jua lakini pia ni moja ya njia ya kuongeza mvuto na muonekano. Hivyo kukufanya kuwa wakipekee. Hii huficha aina za nywere za mtu hasa kwa wenye "brown hair" kwani aina hio ya nywere huwa na muonekano wa mpauko.

3. PIGA PICHA KATIKA MAZINGIRA MAZURI.


Hakikisha mahali unapopigia picha kuna mandhari mazuri yenye kuvutia. Hii hushika "attention" ya watazamaji wa picha zako hata kama mtu hakua na nia ya kuangalia picha yako atajikua amevutiwa na mandhari uliyopigia picha. Hivyo hii kitu inakuongezea point katika muonekano wa picha zako.
 

4. TAFUTA POZI ZENYE KUTEKA HISIA WAKATI WA KUPIGA PICHA:
Kila upigapo picha jitahidi kutafuta pozi ambalo litashika na kuteka hisia za watu. Aina ya pozi izingatie aina ya ujumbe ambao unataka kuufikisha katika jamii unayotaka ikuone
 

UTANGULIZI:
Sehemu hii ni muhimu na yakipekee Kutokana na uhitaji Mkubwa wa jamii hasa kizazi cha vijana kutaka kuwa na muonekano mzuri, mvuto na kusaka heshima ya uvaaji juu ya wenzao.
Hii itakufungua na kukujuza mengi juu ya masuala ya ubunifu wa kimavazi yenye kukupatia muonekano mzuri.


Je !unataka picha nzuri kwa ajili ya mitandao ya kijamii kama FACEBOOK, INSTAGRAM na DP za WHATSAPP???
Soma nakala hii na upate kujua mengi na siri za muonekano wako mzuri uliofichika.



       Imeandaliwa na.......
                                   Denis Kisha Kato (Denis Model)

0 comments:

Post a Comment