Akitoa ufafanuzi wa hoja za walio wachache katika
kamati namba 12, Mbatia alisema ni hatari sana, kuingizwa ushabiki na
propaganda kwa masuala muhimu kama Katiba ambayo yanahusu masilahi ya
taifa.
Mbatia alisema wajumbe waliowengi, hawasomi
nyaraka na kumbukumbu mbalimbali, ambazo zinazungumzia mambo ya
Muungano, badala yake wamekuwa wakitoa taarifa zisizosahihi na kushindwa
kujenga hoja.
“Inashangaa sana kuna wasomi hapa na maprofesa,
wanatoa takwimu potofu na ndiyo hawa ambao walimpotosha hata Rais Jakaya
Kikwete alipokuja kuzindua Bunge la Katiba kwa kutoa takwimu zisizo
sahihi”alisema.
Mbatia alitupia lawama kwa kituo cha Utangazaji
cha Taifa (TBC), kwa kukubali kuonyesha ibada ya kumwombea kifo,
iliyoandaliwa na vijana walioandaliwa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
ndani ya miaka mitano, Jaji Joseph Warioba kiongozi ambaye anaheshimika
ndani na nje ya nchi.
Alifafanua kuwa, baadhi ya wajumbe kwa kutosoma,
wamekuwa wakitioa taarifa potofu juu ya Serikali ya Tanganyika, kuwa
tayari ilifutwa lakini hawajui hata katika katiba ya sasa Serikali ya
Tanganyika inatajwa.
0 comments:
Post a Comment