LICHA ya hivi karibuni gazeti dada la hili, Risasi kumnukuu mcheza filamu mahiri Vincent Kigosi ‘Ray’ akikana kuwepo kwa mpango wa kumuoa mpenzi wake Chuchu Hans, dada huyo ambaye pia ni msanii wa fani hiyo, ameibuka na kusema piga ua lazima wataoana.
Akizungumza na gazeti hili juzikati, Chuchu alisema hana uhakika kama mpenzi wake huyo alimaanisha kile kilichoandikwa gazetini kwa vile ana mapenzi ya dhati kwake.
“Kiukweli mimi moyo wangu unakataa kama alisema maneno hayo kwa vile ni mtu ambaye namjua ana mapenzi ya dhati kwangu,” alisema.
Mwanadada huyo aliongeza kuwa, anahisi kuna kidudu mtu mwenye nia ya kuleta mtafaruku ndani ya uhusiano wao kwa kuchochea fitina ili mapenzi yao yavurugike.
“Unajua kuwa kuna uwezekano kabisa kuna kidudu mtu ambaye anataka kuleta mtafaruku ili tugombane bila sababu na hilo mimi sikubaliani nalo,” alisema.
0 comments:
Post a Comment