KAMATI
ya Uendeshaji ya EURO 2016, Kombe la Mataifa ya Nchi za Ulaya,
imekutana Mjini Paris, Ufaransa na kutangaza Ratiba ya Mechi za Fainali
zitakazochezwa Nchini France Mwaka 2016.
Kamati hiyo inahusisha Wahusika wote
wakuu wakiwemo UEFA, FFF, Shirikisho la Soka la France, Serikali ya
Ufaransa na Miji Wenyeji wa Fainali hizo na kwenye Kikao chao, Rais wa
UEFA, Michel Platini, pia alihudhuria pamoja na Mwenyekiti wa Kamati,
Jacques Lambert na Waziri wa Michezo wa France Najat Vallaud-Belkacem.
Fainali za EURO 2016 zitaanza kwa Mechi
ya Ufunguzi itakayohusisha Wenyeji France itakayochezwa hapo Ijumaa Juni
10 huko Stade de France, Jijini Paris.
Uwanja huohuo ndio utachezwa Fainali
hapo Julai 10, na hiyo itakuwa Mechi ya 51 ya Fainali hizo
itakayoshirikisha Jumla ya Nchi 24 kwa mara ya ya kwanza.
Kabla ya kupata Nchi hizo 24 zitakazotinga Fainali, Nchi za Ulaya inabidi zicheze Mechi za Makundi.
UEFA ilishatangaza Ratiba yote ya Mechi za Makundi ya EURO 2016 ili kusaka Timu 24 zitakazocheza Fainali huko Nchini France Mwaka 2016.
Mechi za Makundi zitaanza Septemba 7, 2014.
Pia, kwa mara ya kwanza, France, ambao
ni Wenyeji wa Mashindano haya, watashiriki Mechi za Makundi, wakiwa
Kundi I, lakini wao hawatapewa Pointi na Mechi zao zitahesabika kama za
Kirafiki tu.
MAKUNDI:
KUNDI A: Netherlands, Czech Republic, Turkey, Latvia, Iceland, Kazakhstan.
KUNDI B: Bosnia-Hercegovina, Belgium, Israel, Wales, Cyprus, Andorra.
KUNDI C: Spain, Ukraine, Slovakia, Belarus, FYR Macedonia, Luxembourg.
KUNDI D: Germany, Republic of Ireland, Poland, Scotland, Georgia, Gibraltar.
KUNDI E: England, Switzerland, Slovenia, Estonia, Lithuania, San Marino.
KUNDI F: Greece, Hungary, Romania, Finland, Northern Ireland, Faroe Islands.
KUNDI G: Russia, Sweden, Austria, Montenegro, Moldova, Liechtenstein.
KUNDI H: Italy, Croatia, Norway, Bulgaria, Azerbaijan, Malta.
KUNDI I: Portugal, Denmark, Serbia, Armenia, Albania.
Timu mbili za juu toka kila Kundi pamoja
na Timu moja Bora iliyoshika Nafasi ya 3 kwenye Makundi zitatinga
Fainali na Timu 8 zilizobaki ambazo zitamaliza Nafasi ya Tatu
zitapangiwa Mechi maalum za Mchujo ili kupata Timu 4 za mwisho kuingia
Fainali.
Mechi za Makundi zitaanza Septemba 2014 hadi Oktoba 2015 na Ratiba kamili itatolewa na UEFA baada ya Droo.
Fainali za UEFA EURO 2016 zitachezwa
Nchini Ufaransa kuanzia Juni 10, 2016 hadi Julai 10, 2016 na kwa mara ya
kwanza Fainali hizo zitakuwa na Nchi 24 badala ya zile 16 za kawaida.
UEFA EURO 2016-SAFARI KUELEKEA FAINALI:
7 Septemba 2014: Mechi za Makundi kuanza
Machi 2015: Tiketi za Fainali kuanza kuuzwa
12 Desemba 2015: Droo ya Mechi za Fainali
Machi 2016: Warsha ya Washiriki wa Fainali
10 Juni 2016: UEFA EURO 2016 inaanza
10 Julai 2016: UEFA EURO 2016 Fainali
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari za michezo kwa muda muafaka bila zengwe
0 comments:
Post a Comment