Facebook

Thursday, 24 April 2014

Ferguson kushiriki mchakato wa kuchagua kocha mpya Mana Utd..................soma hapa................

FERGIE_NA_WANAWE12


SIR ALEX FERGUSON atashiriki kikamilifu katika mchakato wa kumpata Meneja mpya wa Manchester United kuziba nafasi ya David Moyes aliefukuzwa.
Moyes, ambae alipendekezwa na Sir Alex Ferguson ili kumrithi baada ya yeye kustaafu, alifukuzwa kazi Jumanne baada ya kudumu Miezi 10 tu.
Safari hii, Ferguson atakuwa mmoja wa Watu kadhaa, hasa Wakurugenzi wa Bodi ya Man United, watakaoshiriki mchakato mzima wa kumpata Meneja mpya badala ya yeye pekee kupendekeza Jina kama alivyofanya alipoteuliwa Moyes.
Hivi sasa Man United inaongozwa na Meneja wa Muda, Ryan Giggs, ambae ni Kocha-Mchezaji wa Klabu hiyo na anasaidiwa na Wachezaji wenzake wa zamani Nicky Butt, aliekuwa akifundisha Timu ya kikosi cha pili na Phil Neville, aliekuwa Msaidizi chini ya Moyes lakini hii Leo imetajwa kwamba Paul Scholes nae amejumuika kwenye Jopo hilo la Benchi la Ufundi.
Pia, Man United imesema inaendelea kuchambua yupi atafaa kuwa Meneja wao wa kudumu huku Vyombo vya Habari huko England vikigusia kuwa wenye nafasi kubwa ni Kocha wa Netherlands, Louis van Gaal na Meneja wa sasa wa Real Madrid, Carlo Ancelotti.

Related Posts:

  • De Gea mbioni kusaini mkataba mpya Man United.Tetesi zinazovuma hivi sasa ni kwamba Manchester united inategemea kumpa David De Gea mkataba mpya kwa muda miaka 4 ambao unathamini ya £250,000 kwa wiki muda wowote kuanzia hivi sasa. Leo hii amehudhuria katika hafla ya… Read More
  • Yaya Toure njia nyeupe kujiunga Inter Milan.Makamu wa rais wa Inter Milan ya Italia, Javier Zanetti amedai kuwa klabu hiyo inakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa Manchester City Yaya Toure, 32. Klabu hiyo ya Seria A, ambayo inafunzwa na maneja wa zamani … Read More
  • Xavi kuwaaga mashabiki wa Barcelona Alhamisi.KIUNGO mahiri wa kimataifa wa Hispania, Xavi anatarajia kutangaza uamuzi wake wa kuondoka Barcelona Alhamisi hii wakati akijiandaa kuhamia katika klabu ya Al Sadd ya Qatar. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 35 amekuwa akiitumik… Read More
  • Schneiderlin mbioni kuondoka Southampton kwa dau la Paundi Milioni 25.KLABU ya Southampton inatarajia kutaka kitita cha paundi milioni 25 kwa ajili ya kiungo Morgan Schneiderlin mbaye anawindwa na klabu za Arsenal na Tottenham Hotspurs. Klabu hizo zinazotoka kaskazini mwa jiji la London, zote z… Read More
  • Golikipa Peter Cech mbioni Arsenal.Wakati Arsene Wenger akikanusha kutaka kumsajili Petr Cech, wakala wa kipa huyo, Viktor Kolar amethibitisha kwamba Arsenal ni miongoni mwa klabu tatu ambazo mlinda mlango huyo wa Chelsea angependa kujiunga. Kolar amesema klab… Read More

0 comments:

Post a Comment