Thursday, 24 April 2014
Hatimaye Jaji Warioba afunguka leo.....adai amesikitishwa na kauli mbalimbali za viongozi wa CCM
Hatimaye Jaji Warioba amefunga na kusikitishwa na upotoshaji mkubwa sana unaendeshwa na viongozi wa CCM juu ya Rasimu ya katiba.
Amesema kuna uongo unaokuzwa kuwa Serikali tatu inasababisha jeshi kuchukua nchi, amesema kwanini iwe jeshi tu na wasiwe walimu nk?
Akaendelea kusema kuwa akiwa Waziri mkuu mara zote alipokuwa akifanya ziara mikoani alikuwa akitembelea maeneno yenye kambi za jeshi, anasema kulikuwa na hali ngumu sana lakini bado wanajeshi wale waliendelea kufanya kazi kwa weledi mkubwa. Anajiuliza Je, kwanini awakupindua nchi wakati huo.
Amesema kinachosikitishwa ni kauli hizi kutolewa ndani ya makanisa na sehemu za ibada, jambo ambalo amesema kuwa linaweza kuwa ni kuwagawa watanzania kwa itikadi za dini nk.
Jaji Warioba akiwa na uso unaonyesha huzuni amesema kuwa wanasiasa na hasa wa chama tawala wanaweza wakalipasua Taifa na kuleta madhara makubwa kwa Taifa mbeleni
Related Posts:
Hotuba ya Mh.Edward Lowassa akitangaza nia kugombea Urais kupitia CCMHOTUBA YA MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA KWENYE MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI KWA AJILI YA KUTANGAZA NIA YA KUOMBA KUTEULIWA KUWA MGOMBEA WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) KWA NAFASI YA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA UTANGUL… Read More
Wanachuo wapindua Serikali yao UDOM.Wanafunzi wa kitivo cha elimu katika chuo kikuu cha Dodoma wameipindua serikali ya wanafunzi wa kitivo hicho kwa madai ya kutowajibika kwa viongozi pamoja na madai ya ubadhirifu wa fedha. Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM). Mapinduz… Read More
BantuTz MAGAZETINI:Soma kilichoandikwa katika kurasa za magazeti yote ya leo Jumatatu,Juni 1. MAGAZETINI-Ni uratatibu ambao BantuTz imeuanzisha ili kuwawezesha wadau wote wa Bantu waweze kusomana kupitia kurasa za magazeti mbalimbali nchini kila siku asubuhi ili kuwasogezea karibu zaidi huduma kupata habari nuh… Read More
BantuTz MAGAZETINI:Soma kilichoandikwa katika magazeti yote ya leo Jumanne,Juni 2. MAGAZETINI-Ni uratatibu ambao BantuTz imeuanzisha ili kuwawezesha wadau wote wa Bantu waweze kusomana kupitia kurasa za magazeti mbalimbali nchini kila siku asubuhi ili kuwasogezea karibu zaidi huduma kupata habari nuhimu… Read More
BantuTz MAGAZETINI:Soma kilichoandikwa katika kurasa za magazeti yote ya leo Jumapili,Mei 31 MAGAZETINI-Ni uratatibu ambao BantuTz imeuanzisha ili kuwawezesha wadau wote wa Bantu waweze kusomana kupitia kurasa za magazeti mbalimbali nchini kila siku asubuhi ili kuwasogezea karibu zaidi huduma kupata habari nuhimu… Read More
0 comments:
Post a Comment