Arudisha desturi zote za Sir Alex Ferguson
LEO hii, Ryan Giggs atafanya Mkutano wake wa kwanza na Wanahabari tangu ateuliwe kuwa Meneja mpya wa Manchester United.
Giggs aliteuliwa Siku ya Jumanne mara
baada ya David Moyes kufukuzwa na Mkutano huo wa Leo utafanyika Saa 6
Mchana, Saa za Bongo, huko Aon Training Complex, Jijini Manchester
ambako ndio Kituo cha Mazoezi cha Man United.
Giggs, mwenye Miaka 40, atafanya Kikao
hicho kwenye chumba kilekile alichokuwa akitumia Sir Alex Ferguson kwa
Mkutano wake wa kila Wiki tofauti na David Moyes aliekuwa akitumia
Ukumbi mwingine.
Pia, kama alivyokuwa Sir Alex Ferguson,
Giggs ameurudisha Mkutano huo wa kila Wiki wa Waandishi wa Habari,
unaofanyika kila Ijumaa, kufanyika Asubuhi kabla ya kuanza Mazoezi
wakati Moyes alikuwa akiufanya baada ya Mazoezi.
Mechi ya Kwanza ambayo Giggs atasimamia
kama Meneja, akisaidiwa na Nicky Butt, Paul Scholes na Phil Neville, ni
Jumamosi Uwanja wa Old Trafford dhidi ya Norwich City kwenye Ligi Kuu
England.
Tayari Giggs ameshawataka Wachezaji wake
kurudia kucheza kama Manchester United kwa kuzishambulia na kuzibana
Timu kama walivyokuwa wanafanya chini ya Sir Alex Ferguson.
Giggs ataisimamia Man United kwa Mechi zao 4 za Ligi zilizobaki Msimu huu.
0 comments:
Post a Comment