WAKUSANYAJI
wa Stika huko Jijini Rio De Janeiro, Brazil walipatwa na mstuko baada
ya Gari lillilobeba Maelfu ya Stika za Aina ya Panini kuibiwa zikiwemo
zile za Mastaa wakubwa Cristiano Ronaldos, Lionel Messis na Neymar.
Stika 300,000 zilizokuwemo ndani ya Gari hilo zilikuwa zikisambazwa kwenye Maduka yanayouza Magazeti ili Wakusanyaji wazinunue.
Stika hizo zenye Picha mbalimbali za
Mastaa watakaocheza Fainali za Kombe la Kombe la Dunia huko Brazil Mwezi
Juni hukusanywa na Washabiki na kubandikwa kwenye Vitabu au Ukutani.
Stika hizi za Aina ya Panini zilianza kutumika kwenye Fainali za Kombe la Dunia la Mwaka 1970.
Hata hivyo, Kampuni ya Panini
imewahakikishia Washabiki kuwa zipo Stika za kutosha kwa wao kukamilisha
idadi ya Stika 640 ambazo ndio za Wachezaji wote wakiwemo wale Masta
wakubwa kabisa Cristiano Ronaldos, Lionel Messis na Neymar.
Hivi sasa Stika hizo ni maarufu mno huko
Nchini Brazil ambako ndiko Fainali za Kombe la Dunia zitachezwa kuanzia
Juni 12 hadi Julai 13 Mwaka huu.
Umaarufu wa Stika hizi umakua sana kiasi
ambacho Watu, Vijana kwa Wazee, huingia Mitandaoni na kubadilishana
Stika ili kutimiza Idadi ya Stika 640 ambazo ndio hufanya Albamu moja.
Kampuni ya Panini imesema inatarajia kuuza Albamu Milioni 8 huko Brazil.
Hii si mara ya kwanza kwa Stika za
Panini kuibiwa kwani Mwaka 2010 huko Afrika Kusini, kabla kuanza kwa
Fainali za Kombe la Dunia, Wezi walivamia Kituo cha Ugawaji wa Stika na
kuzoa Paketi 135,000 lakini baadae zilikamatwa.
0 comments:
Post a Comment