Facebook

Sunday 24 August 2014

Teknoilojia ya Hali ya Juu;Adidas watoa mpira wenye "SENSA"


Kampuni ya adidas wametoa mpra wa miguu ambao una uwezo wa kutoa takwimu za mchezaji na kupeleka kwenye gajaeti za iOS, yaani iPhone,iPad na iPod Touch kwa kutumia app ya Micoach. Mpira huo unajulikana kama Micoach Smart Ball una sensa mbali mbali ikiwemo bluetooth.

Mbali na mpira huo kuchukua takwimu kwa ajili ya kuchambua
uchezaji wako, kasi ya mashuti, jinsi unavyopindisha free kick na
kadhalika app ya mpira huo pia hutoa maelekezo mbali mbali ambayo yatasaidia jinsi unavyocheza mpira, hasa katika mambo kama vile freekick kona na kupiga mashuti. 


Miongoni mwa mambo maalum yanayofundishwa na app ya Micoach ni jinsi ya kuumudu mpira (ball mastery), kupiga mpira (ball striking), kupiga mashuti (striking with power) na jinsi ya kupindisha au kuvusha mpira kwenye ukuta wa freekick (around the wall na over the wall).

Hivyo takwimu ambazo utazipata zinakuwa kama vile kasi ya shuti lako ni 70 mph ma spin ni 48 rpm. 
Hivyo hii Micoach smart ball pia itakuwezesha kujua ni kiasi gani
unaweza ku-spin mpira na kwa kasi gani. Mbali ya hayo pia inataoa
takwimu zinazoweza kuonyesha umahiri wa kipa na hata ubora wa
pasi zako. Mpria huo una chaji isiyo na waya na pia una kisahani (cradle) cha kuchajia.


Mshambuliaji wa Spain na Man City Alvaro Negredo akiwa na Micoach Smart Ball Adidas ndio kampuni rasmiitakayotengeneza mipira itakayotumika kwenye Kombe la Dunia huko Brazil mwaka huu.
Micoach smart ball utauzwa kwa $299 za kimarekani. Mipira hii
itauzwa na Adidas wenyewe pamoja na maduka karibu mia nne ya Apple.

0 comments:

Post a Comment