Facebook

Sunday, 24 August 2014

Chelsea yazidi kupaa kileleni.


Costa ameandikisha bao lake la pili katika ligiku ya Uingereza
Mshambulizi wa Uhispania Diego Costa aliifungia Chelsea bao lake la pili katika mechi mbili na kuisaidia the Blues kuilaza Leicester mabao 2-0 katika mechi yao ya kwanza ya nyumbani Stamford Bridge.

Kipindi cha kwanza ilikuwa nipe nikupe kati ya vijana wa Mourinho na mabingwa msimu uliopita wa ligi ya daraja la pili.
Kipa mgeni Stamford Bridge Thibaut Courtois alifanya kazi ya ziada na kudhihirisha kwanini mkufunzi Jose Mourinho alimteua kuanza langoni badala yake kipa Petr Cech.
Hata hivyo hakuna yeyote aliyewahi kufunga mwenzake bao katika kipindi cha kwanza.

Hata hivyo katika kipindi cha pili ni mshambulizi huyo kutoka Uhispania aliyetokea Atletico Madrid aliyecheka na wavu na kuibua shangwe uwanjani Stamford Bridge.
Hazard aliifungia Chelsea bao la pili.
Costa alitumia pasi safi ya Branislav Ivanović katika eneo la lango na kutikisa wavu kunako dakika ya 63 ya kipindi cha pili.
Leicester walijifurukuta na kufanya mashambulizi dhidi ya Chelsea lakini utepetevu wa mshambulizi wao wa kutegemewa David Nugent
uliwanyima fursa hiyo ya kipekee.
Vijana wa Mourinho waliendeleza mashambulizi hayo na juhudi zao zikazawadiwa kunako dakika ya 77 Eden Hazard alipofuma mkwaju kimiani na kumwacha kipa Kaspar Schmeichel asijue iliipitia wapi.
Bao hilo linamaanisha Chelsea wamesajili ushindi wao wa pili katika mechi yao ya pili msimu huu.
Katika matokeo mengine ya leo Aston Villa ilitoka sare tasa na Newcastle
West Ham ikaiadhibu vikali Crystal Palace mabao 1 - 3 .
Southampton walitoka sare tasa na West Brom huku Swansea ikiendeleza msururu wa matokeo mema kwa kuibana
Burnley 1-0.

Related Posts:

  • Baada ya "Magumashi" Evodius Mtawala aachia ngazi TFF Mkurugenzi wa wa Vyama na Masuala ya Kisheria katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Evodius Mtawala, amelazimika kuachia ngazi kutokana na sababu mbalimbali. Taarifa ambazo tumezipata, zinaeleza kuwa Mtawala ambaye aliwah… Read More
  • Wenger apanda ndege kuelekea Roma,Italy Arsene Wenger ameonekana akipanda ndege kutoka London kwenda Rome, Italy. Meneja huyo amekubali kuwa meneja wa timu itakayocheza mechi maalum ya amani, katika mchezo wa soka wa unaojumuisha imani mbalimbali ulioandaliwa na P… Read More
  • HAYA NDO MAPYA YALIYOBUKA OLD TRAFORD KUHUSU ROJO Mlinzi Marcos Rojo aliyesajiliwa Manchester United kutoka Sporting Lisbon ya Ureno anakabiliwa na shauri la jinai kwao Argentina, na ndilo linamzuia kuanza kuchezea timu yake mpya. Hadi Jumapili hii asubuhi alikuwa hajapatiw… Read More
  • Wachezaji waliosajiliwa kwa bei ghali msimu huu 2014/151. Luis Suarez €88m 2. James Rodriguez €80m 3. Angel di Maria €75m 4. David Luiz €49.5m 5. Eliquim Mangala €44.5m 6. Diego Costa €44m 7. Alexis Sanchez €40m 8. Luke Shaw € 37.8 … Read More
  • Usajili kamili wa Simba msimu huu Makipa: Ivo Mapunda na Hussein Shariff ‘Casillas’. Mabeki: Joseph Owino, Donald Mosoti, Abdi Banda, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Said Nassoro Masoud ‘Chollo’, Joram Mgeveke na William Lucian ‘Gallas’, Viungo: Pierre Kwizera… Read More

0 comments:

Post a Comment