Facebook

Saturday, 19 April 2014

Chelsea yafungwa darajani,Tottenham yaua.......fuatilia hapa uchambuzi wa mechi zote za leo EPL................





Chelsea 1-2 Sunderland Fc.
Rekodi nzuri ya Jose Mourinho ya kutofungwa katika Mechi 78 za Ligi Kuu England Uwanjani Stamford Bridge Leo imevunjwa baada ya kuchapwa Bao 2-1 na Timu ya mkiani Sunderland na kuyaacha matumaini yao kutwaa Ubingwa mashakani huku Vinara Liverpool wakichekelea.
Sunderland bado wako mkiani lakini Jumapili, Liverpool wakishinda watakuwa Pointi 5 mbele juu kileleni na kubakiwa na Mechi 3 mojawapo ikiwa Wikiendi ijayo Uwanjani Anfield na Chelsea na hapo wanaweza kabisa kutwaa Ubingwa kutegemea na Mechi nyingine kabla ya hiyo.
Leo hii, Chelsea walitangulia kufunga kwa goli la Samuel Eto’o na Sunderland kusawazisha kwa goli hilo kupitia kwa Connor Wickham.
Goli la ushindi kwa Sunderland lilifungwa kwa Penati ambayo Msaidizi wa Refa ndie alimuashiria Refa Mike Dean ni Penati baada ya beki wa kushoto wa Chelsea Azpilicueta kuteleza na Mpira kunaswa na Altidore ambae aliingia ndani ya Boksi na Azpilicueta kujaribu kuuzuia Mpira lakini Altidore akajiangusha na Penati kutolewa.
Penati hiyo ilifungwa na Borini.


Tottenham 3 Fulham 1
-White Hart Lane
Bao za Paulinho, Kane na Kaboul zimewapa Tottenham ushindi wa Bao 3-1 walipocheza na Fulham ambao kipigo hiki kimezidisha wasiwasi wao wa kushushwa Daraja.
Bao pekee la Fulham lilifungwa na Steve Sidwell ambae pia alikosa Penati iliyookolewa na Kipa Hugo Lloris.


Cardiff City 1 Stoke City 1
-Cardiff City Stadium
Golio za Penati zimeifanya Mechi hii imalizike kwa Sare ya goli 1-1
Marko Arnautovic aliifungia Stoke kwa Penati iliyotolewa kwa Faulo ya Kim Bo-Kyung kwa Peter Odemwingie na Peter Whittingham kusawazisha kwa Penati kwa faulo iliyofanywa  na Steven Nzonzi kwa Fraizer Campbell.

Newcastle United 1 Swansea City 2
-Saint James’ Park
Penati ya Dakika za Majeruhi ya Wilfried Bony imeipa ushindi wa magoli 2-1 Swansea City walipocheza Ugenini na Newcastle na kuwapa matumaini makubwa ya kunusurika kushushwa Daraja.
Newcastle ndio walitangulia kwa goli la Shola Ameobi lakini Wilfried Bony alisawazisha.
Wakati Mechi ikielekea kuwa Sare, katika Dakika za Majeruhi Marvin Emnes aliangushwa na Cheick Tiote ndani ya Boksi na Bony kufunga goli lake la Pili na la ushindi.
Refa Chris Foy ilibidi atolewe katika Dakika ya Kwanza baada ya Shuti la Jonjo Shelvey kumbabatiza Usoni na nafasi yake kuchukuliwa na Refa wa Akiba, Anthony Taylor.

 West Ham United 0 Crystal Palace 1
-Upton Park
Crystal Palace wamejihakikishia kubaki Ligi Kuu Engkand baada ya kuichapa West Ham United, waliokuwa kwao Upton Park, goli 1-0 kwa Penati ya Mile Jedinak ya Dakika ya 59 iliyotolewa kufuatia Pablo Armero kumwangusha Cameron Jerome.
 
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari za uhakika kwa muda muafaka......
 
 
 

Related Posts:

  • Ratiba ya Mechi za Ligi kuu Uingereza Septemba 19 na 20.Kesho Jumamosi Septemba 19 14:45 Chelsea vs Arsenal 17:00 Aston Villa vs West Brom 17:00 Bournemouth vs Sunderland 17:00 Newcastle Utd vs Watford 17:00 Stoke City vs Leicester 17:00 Swansea vs Everton 19:30 Manchester City vs… Read More
  • Wenger akataa kuzungumzia suala la yeye kushikana mkono na Mourinho.Arsene Wenger leo amegoma kuweka wazi kama atapeana mkono na Jose Mourinho lakini ameweka kando juu ya umuhimu wa uhusiano wao kutokwenda vizuri kuelekea ziara ya Arsenal kwenda kuwatembelea Chelsea. Mameneja hao wawili walio… Read More
  • Real Madrid yamnasa mkimbizi Osama.Soka limetumika sana kusambaza upendo kwenye ishu ya wakimbizi wa Syria ambayo imetoka wiki chache zilizopita. Stori ya mkimbizi huyu Osama Abdul Mohsen ambapo video yake ilisambaa akiwa amembeba mwanae anakimbia huku mpiga p… Read More
  • YANGA YATUMA SALAMU MSIMBAZILigi Kuu ya Tanzania Bara imeendelea leo kwa kushuhudia viwanja vinne vikiwaka moto, ambapo katika uwanja wa Taifa Dar es salaam, mabingwa watetezi Yanga wamepata ushindi wa tatu mfululizo kwa kuichapa JKT Ruvu mabao 4-1. Mab… Read More
  • Kerr : Kumbe Simba SC walinidanganya kuhusu MgamboTanga. Kocha wa Simba, Dylan Kerr amefichua siri ambayo ni vigumu kuiamini. Alisema alilazimika juzi kupanga viungo wengi dhidi ya Mgambo JKT kutokana na kupewa taarifa kuwa timu hiyo inacheza soka la kushambulia kwa wakati w… Read More

0 comments:

Post a Comment